Shekh Ponda.
Polisi mkoani
Morogoro imemtaka Shekh Ponda Issa Ponda kujitokeza mbele ya Jeshi hilo
kuthibitisha taarifa za kupigwa risasi katika tukio lililotokea baada ya
kongamano lililoandaliwa na wahadhiri wa dini ya kiislamu.
Taarifa
zinadai kuwa shekh Ponda alipigwa risasi begani majira ya saa 12 jioni baada ya
kongamano hilo wakati akisindikizwa na wafuasi wake wa dini ya kiislamu
kuelekea katika msikiti wa mungu mmoja dini moja.
Shekh Ponda
Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro Faustin Shilogile amesema polisi wakiwa katika harakati za kumkamata Shekh Ponda kwa makosa ya uvunjifu wa masharti aliyopewa na mahakama, walifyatua risasi za baridi kuwatawanya wafuasi waliokuwa wakisukuma gari la sheikh Ponda.
This comment has been removed by the author.
ReplyDelete