Prof. Ibrahim Lipumba
Dar es Salaam.
Katibu wa
Jumuiya na taasisi za kiislam nchini Sheikh Ponda Issa Ponda anayedaiwa kupigwa
risasi na polisi mkoani morogoro mara baada ya kumalizika mhadhara aliokuwa
akihutubia, amelazwa chini ya uangalizi katika hospitali ya taifa Muhimbili kwa
ajili ya matibabu.
Taarifa za
kulazwa kwa kiongozi huyo zimetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF
Profesa Ibrahim Lipumba, ambaye alikwenda kumjulia hali hii leo.
Sheikh Ponda Issa Ponda
Prof. Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada
ya kumtembelea katika wodi ya dharura katika hospitali ya taifa ya Muhimbili
amesema tukio hilo ni miongoni mwa matukio mabaya yanayodaiwa kufanywa na
vyombo vya dola ambayo hayana budi kudhibitiwa kwani yanaweza kuwa na madhara
kwa ustawi wa taifa.
"Cama cha Cuf
kinasikitishwa sana na kufadhaishwa na Mwendelezo wa vitendo vya kikatili vya
mauaji ya raia yanayo fanywa na jeshi la polisi kwa kisingizio cha kulinda
amani ya nchi, huu utaratibu au sera ya piga tu tumechoka itatufikisha pabaya alisema Lipumba.
Aidha Prof. Lipumba Amemwomba
Rais Jakaya Kikwete na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini inspekta Jenerali Saidi
Mwema kuhakikisha kuwa matukio ya kupigwa risasi wananchi wasiokuwa na silaha
yanakomeshwa lakini pia wanaohusika kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo
kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Rais Jakaya Kikwete
Hata hivyo Prof.Lipumba amevitahadharisha vyombo vya dola hususan jeshi la polisi
kuhakikisha kuwa linaondoa vizingiti vya kupatiwa matibabu sheikh Ponda ,ambapo
pia amewataka waislam pamoja na wananchi kwa ujumla kuwa na subira wakati
sheikh ponda akiendelea kupatiwa matibabu.
0 comments:
Post a Comment