Baadhi ya
wazee wakiwa wanatafakari jambo, hii nikutokana na wao kuelezwa yakuwa wanao
uwezo mkubwa wa kuwalinda watoto wao dhidi ya vitendo vya ubakaji. (Picha na
Maktaba yetu).
Imebainika kuwa Wazee wanao wajibu mkubwa wa kuwalinda watoto wao dhidi ya vitendo vya
ubakaji, hasa katika kipindi hichi cha baada ya mfunguo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kauli hiyo inatokana na Takwimu zinaonesha kuwa
katika miezi ya kawaida, watoto wengi hukabiliana na vitendo vya udhalilishaji
wakiwamo wale wanaotembea maeneo hatarishi wakiwa peke yao.
Taarifa kutoka Chama cha Wanawahabari Wanawake
Tanzania (Tamwa) upande wa Zanzibar, imesema kuwa hivi karibuni, msichana wa
miaka 12 (jina linahifadhiwa) alibakwa sehemu alipokuwa akitafuta kuni huko
Kianga, wilaya ya kati, Unguja.
Msichana huyo anadaiwa kubakwa na kupata maumivu
makali yaliyomsababishia kulazwa katika hospitali ya rufaa ya Mnazimmoja.
Taarifa iliyosainiwa na Mratibu wa Chama hicho
Zanzibar, Mzuri Issa, ilisema ni vyema wazazi kuwaambatanisha watoto hao na
watu wazima ili kuwapunguzia mwanya wabakaji.
Taarifa hiyo Iliainisha vitendo vya ubakaji vinavyotokea katika maeneo hayo hatarishi yakiwamo kwenye misitu na giza, kwani ilikuwa.
Kwa namna
hii kwa Pamoja tukishirikiana Tunao uwezo wa kutokomeza vitendo vya ubakaji kwa
watu wanamna hii dhidi ya wanawake na watoto.
(Picha na Maktaba yetu).
0 comments:
Post a Comment