Semvua Musangi.
Ofisi ya Mbunge wa Ilala kwa kushirikiana na Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania TRA wanakamilisha ukarabati wa mfumo wa miundombinu ya
maji safi katika makazi ya askari Polisi wa kituo cha Msimbazi kilichopo
Kariakoo jijini Dar es Salaam, ili kuongeza ufanisi wa upatikanaji wa maji
kwenye makazi hayo yaliyopo kwenye jengo la gorofa.
Akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Chama cha
Mapinduzi CCM Kata ya Kariakoo kuangalia maendeleo ya Mradi huo, Katibu wa
Siasa na Uenezi wa Chama hicho kata ya kariakoo Halima Abdallah amesema mradi
huo ambao ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM, upo katika hatua za mwisho
kukamilika.
Halima Abdallah Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama.
Amesema mkandarasi anayefanya kazi hiyo atahakikisha
maji ya bomba ambayo kwa sasa yanapatikana chini pekee yatapandishwa hadi
kwenye gorofa hizo, ili kila wakazi waliopo kwenye gorofa husika wanapata
huduma hiyo walipo badala ya kulazimika kushuka hadi chini kuteka maji.
Naye Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kipolisi ya Kariakoo
Filbert Luhanyula amesema anaamini mradi huo utaleta nafuu kwa familia za
askari wanaoishi kwenye jengo hilo ambao kwa sasa wanapata usumbufu wa
kupandisha maji juu kwa kutumia ndoo na madumu.
Filbert Luhanyula Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kipolisi ya Kariakoo
Kondo Thabit - Mwenyekiti wa
Serikali za Mitaa - Kariakoo Kaskazini.
Mradi huo unaotekelezwa kwa gharama ya zaidi ya Shilingi Milioni nane na laki nane, utanufaisha Jumla ya familia themanini za askari polisi wanaoishi kwenye jengo hilo la gorofa nne.
0 comments:
Post a Comment