Rais Barack Obama amekosoa barua ya maseneta wa chama cha Republican iliyotumwa kwa Iran, na kukituhumu chama hicho kwa kuingilia mazungumzo ya kusitisha urutubishaji nyuklia.
Rais Obama amesema masetena 47
waliofanya jambo hilo wameunda muungano usiowakawaida na na viongozi
wa dini wenye misimamo mikali.
Barua hiyo imeikumbusha Iran kuwa
makubaliano yoyote yatakayofikiwa na serikali kuu, yatakuwa na maana
iwapo yataridhiwa na baraza la Congress ambalo linaongozwa na chama
cha Republican.
Mazungumzo ya mpango wa kurutubisha
nyuklia wa Iran upo katika hatua muhimu, huku muongozo wa makubaliano
hayo ukitarajiwa kutolewa Machi 31.
0 comments:
Post a Comment