Image
Image

Breaking News:Mh.Kassim Majaliwa ameteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.


Rais Dokta John Pombe Magufuli amemteua mbunge wa Ruangwa wa chama cha mapinduzi CCM Kassim Majaliwa Kassimu kuwa waziri Mkuu katika serikali yake ya awamu ya tano ambapo jina lake limetangazwa na Spika wa bunge Mh.Job Ndugai kwa wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bungeni mjini Dodoma.

Mh.Kassim Majaliawa ambaye aliingia katika medani ya siasa mwaka 2010 baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa Ruangwa na kuteliwa kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ambapo katika serikali ya awamu ya nne ya rais Jakaya Kikwete,Mh.Kasim Majaliwa Kasim alikuwa naibu waziri wa ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEM anayehudumia elimu.

Uteuzi wa Mh.Kasimu Majaliwa kuwa waziri mkuu utakamilika mara baada ya wabunge wote kumpigia kura ya kumuidhisha na baadaye kuapishwa na rais na kuanza kazi kama kiongozi wa serikali.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment