Ukosefu wa zahanati
katika baadhi ya kata za mji wa shinyanga ikiwemo kata ya Ndembezi na Ngokolo
imetajwa kuwa ni kikwazo kinachosababisha wananchi wa maeneo hayo kutumia muda
mrefu kufuata huduma za afya hali ambayo imekuwa ikisababisha wananchi wa kipato
cha chini kushindwa kumudu gharama za matibabu huku ongezeko la vijana
wanaoshinda vijiweni likiongezeka kutokana na ukosefu wa ajira na miundombinu
ya kujiajiri.
Wakizungumza kwa nyakati
tofauti baadhi ya wananchi wa kata ya Ndembezi iliyoko katika manispaa ya mji
wa Shinyanga wamewataka viongozi walioingia madarakani kuhakikisha zahanati
iliyokuwa imeanza kujengwa kwa nguvu za wananchi inamalizika hali ambayo
itatatua changamoto ya huduma ya afya inayowakabili kwa muda mrefu.
Kwa upande waka diwani Mteule
wa kata ya Ndembezi Bw.David Nkulila wamewahakikishia wananchi wake kuwa
kipaumbele chake cha kwanza baada ya kuapishwa ni kuhakikisha miundombinu ya
barabara na ujenzi wa zahanati unamalizika ili kutatua changamoto za kimaisha
zinazowakabili huku diwani wa kata ya Ngokolo kupitia Chadema Bw.Emmanuel Ntobi
akidai kuanza kuboresha changamoto ya miundombinu ya soko na kutoa elimu ya
ujasiriamali kwa vijana na akina mama ili kuwajengea uwezo wa kujiajiri wenyewe
hali ambayo itaongeza kipato na kupunguza ugumu wa maisha.
0 comments:
Post a Comment