Image
Image

Jamii yatakiwa kutoa ushirikiano kusaidia watoto waishio mazingira magumu Morogoro.

Na.Devotha Songorwa,Morogoro.
Shirika lisilokuwa la kiserikali la Faraja Trust Fund lililopo manispaa ya Morogoro limewataka wanajamii kutoa ushirikiano katika kuwalea watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili kuisaidia jamii inayowazunguka.
Ameyazungumza hayo Afisa tawala wa shirika hilo DAMIANI MUSHI amesema lengo kubwa la shirika hilo ni kuisaidia jamii  ambapo shirika hilo linatoa huduma kwa watoto wa mitaani, pamoja na lishe  kwa upande wa wazazi na watoto.
Akibainisha baadhi ya changamoto zinazowakabili  katika utoaji wa huduma MUSHI amesema kituo hicho kinaukosefu mkubwa wa wafadhili hali inayowapelekea kushindwa kuhudumia jamii kwa kiasi kubwa.
Kwa upande mwingine ameyashukuru baadhi ya mashirika na watu binafsi kwa msaada wanaoutoa na na kutoa wito kwa mashirika na taasisi mbalimbali kuiga mfano huo ili kuwaokoa watoto na wanawake wanaohitaji msaada.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment