Zoezi la ubomoaji limefanywa majira ya asubuhi yaleo
saa tatu huku mmoja wa mwenye nyumba akilaani na kusema kuwa kesi ya suala hilo
iko mahakamani tangia Dec 2 na kushutumu mkurugenzi aliyeagiza uvunjwaji wa
nyumba katika maeneo hayo kuwa kwa kufanya hivyo ipo nguvu ya fedha iliyo
tumika ndio maana zoezi hilo linafanywa kwa nguvu.
Kufuatia malalamiko hayo Tambarare Halisi iliweza
kumtafuta na kuzungumza naye Kamishna Ardhi nchini Dk
Moses Kusiluka ambapo amefafanua kuwa zoezi la uboaji huo
halijaanza leo wala jana ila ni muendelezo na kusema kuwa zoezi hilo
wanalifanya kwa waliokiuka taratibu na sheria kwa kujenga maeneo ya
wazi,wavamizi wa maeneo na kujenga bila kibali na waliokwisha wekewa
alama ya mkasi kuondoka maeneo hayo ambapo eneo la Mwenge walio wengi wamevamia
eneo la wazi na kujenga.
Amesema taarifa za kutakiwa kuondoka maeneo hayo
wanayo hivyo kilichokuwa kikifanyika ni utekelezaji tu wa wao kuondoka na ndio
maana zoezi la ubomoja wamelifanya kwa kuwa wametoa taarifa muda mrefu licha ya
malalamiko kuwa kuna kesi mahaka mani,amesema kuwa kesi hizo hazi wahusu
kwakuwa hazijagfunguliwa kwaajili yao kama wizara.
Katika zoezi la uvunjaji wanafuata sheria na
taratibu kwani zoezi hilo hali mgusi masikini wala tajiri ila kama umekiuka
taratibu na sheria ndio ina fuata mkondo wake.
Ameeleza kwa kina kuwa zoezi hilo ni Endelevu ambapo
linahusisha wilaya tatu za Temeke,Ilala,Kinondoni hivyo akatoa wito kwa
waliokwisha tahadharishwa kuondoka maeneo ambayo sio rasmi wafanye hivyo mara
moja kabla hawajafikiwa na zoezi hilo la ubomoji.
Aidha Dk. Kusiluka ameongeza na kuwaonya watu
wengine ambao wapo maeneo ambayo yashaa katazwa kuchukua hatu mara moja kabla
hawajafikiwa kwa kuwa zoezi hilo wanaenda nalo kwa kasi sana hivi sasa nasiku
zijazo.
Katika siku chache zilizopita zoezi hili la Bomoabomoa
liliwakumba wakazi wa Kidongo Chekundu kurasini jijini Dar es Salaam ambao nao
walikwisha pewa tahadhari ya kuondoka maeneo hayo lakini hawakuchukulia
maanani.
0 comments:
Post a Comment