Hatimaye chama cha mapinduzi CCM kimempitisha
Mhe. Dr.Tulia Ackson Mwansansu kuwa mgombea wa kiti cha unaibu spika wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,.
Katibu wa itikadi na ueneziwa chama hicho Nape Nauye
ameweka wazi mbele ya wanahabari akiwa mjini Dodoma ambambo michakato
mbalimbali inaendelea baada ya kupatikana Spika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ambapo kazi kubwa hivi leo ilikuwa kuwaapisha wabunge waliokuwa
wamebaki kutokana na jana muda kutotosha.
Baada ya Dr.Tulia kupitishwa kuwania nafasi hiyo
sasa atachuana na mgombea mwezie Bi.Magdalena Sakaya kutoka CUF/Kwa umoja wa
Mwavuli wa UKAWA,ambapo hadi sasa haijaelezwa kuwa kuna majina ya wagombea toka
vyama vingine kwaajili ya kugombea na fasi hiyo ya unaibu Spika.
Dr.Tulia awali aliwania nafasi ya uspika na hivyo
kupata bahati ya jina lake kupenyan kama mwana mama pekee katika nafasi
hiyo ambapo halimashauri kuu ya CCM chini ya Dk.Jakaya kikikwete iliwapitisha
wagombea watatu ndani ya chama hicho 1. Mhe Job Ndugai 2. Mhe Abdullah Ali
Mwinyi. 3. Dr Tulia Ackson Mwansasu. Na hivyo mwishowe Dr.Tulia na Ali Mwinyi
kujitoa na kumwachia Mh.Job Ndugai ambaye ameweza kupenya kwenye nafasi ya
uspika wa Bunge na kuchaguliwa kwa kura 254,akifuatiwa na Mpinzani wake
GOODLUCK OLE MEDEYE (CHADEMA) kwa kura – 109 huku wengine wakiwa hawakupata
kitu.
Muda mchache baada ya kujitoa katika kinyang”anyiro
cha kuwania Uspika wa Tanzania Rais.DR.John Pombe Magufuli kwa mamlaka ya
katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara TA 66 ambayo inampa madaraka
rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuteua wabunge 10,alitumia mamlaka hayo
kumteua Dr.Tulia kuwa Mbunge wa kwanza wa Bunge la 11 la Tanzania.
Baada ya uteuzi huo sasa zinasubiriwa taratibu
zingine kwajili ya kupigiwa kura ili mmoja wao kushinda,huku vichwa vya
watanzania vikigonga kutafakara huenda Rais.Magufuli atamchagua nani kuwa
waziri mkuu wa Tanzania na Baraza la mawaziri litakuwa la namna gani kwa mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment