Kesi hiyoambayo ilitarajiwa kutolewa hukumu yake siku
ya jumatano na hakimu mkazi wa mahakama hiyo Mary Moyo imeahirishwa baada
ya hakimu husika kutokuwepo mahakamani hapo kwa madai kuwa amekwenda
kwenye kozi fupi ya kushughulikia kesi za uchaguzi mjini dodoma ambapo
shauri hilo limelazimika kuahirishwa na hakimu mkazi Erick Rwehumbiza
hadi Novemba 30,mwaka huu itakapofikishwa tena mahakamani hapo na mshtakiwa
kurudishwa rumande.
Mshtakiwa huyo anakabiliwa na mashtaka mawili
ikiwemo kutoa maneno yenye kuumiza imani za dini na kushawishi watu
kutenda kosa,mashtaka anayodaiwa kuyatenda agosti mwaka 2013.
Ambapo katika kesi hiyo upande wa mashtaka unawakilishwa wakili wa
serikali mwandamizi benard kongola, sunday hyera na george mbalasa wakati
upande wa utetezi unawakilishwa na wakili juma nasoro, abubakar salim
na bartholomeo tarimo.
Awali hukumu ya sheikh ponda ilipangwa kutolewa 19, 10
kabla ya kuahirishwa tena na shauri hilo kupangwa kutolewa hukumu novemba 18
mwaka huu, kabla ya kuahirishwa tena hadi novemba 30.
0 comments:
Post a Comment