Wakati wa upigwaji wa kura -Idadi ya
wabunge kikatiba walikuwa 394,Wabunge waliosajiliwa 369,Akidi 184,idadi ya
wabunge waliokuwepo ukumbini wakati wa zoezi la kupiga kura 351,Kura
zilizopigwa 351,Kura mbili ziligharibika,idadi ya kura halali zikawa 349,huku idadi
ya kura za hapana 91 sawa na asilimia 25 .9,idadi ya kura zilizo haribika 2
sawa na asilimia 0.06.
Mh.Kassim Majaliawa ambaye Kitaaluma
ni mwalimu aliingia katika medani ya siasa mwaka 2010 baada ya kuchaguliwa kuwa
mbunge wa Ruangwa na kuteliwa kushika nyadhifa mbalimbali serikali ambapo
katika serikali ya awamu ya nne ya rais.Jakaya Kikwete Mh.Kasim Majaliwa Kassim
amewahi kuwa naibu waziri wa elimu na mpaka serikali ya awamu ya nne inamaliza
muda wake alikuwa naibu waziri wa nchi
ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEM anayehudumia
sekta ya elimu.
Mbali na kuwa mbunge pia amewahi kuhudumu kama mkuu wa wilaya Mwaka
2006 hadi 2010, katibu chama cha walimu wilaya na mkoa na Mwalimu.
Je.Kassim
Majaliwa ni nani na ametoka wapi.
Kassim Majaliwa Mbunge wa Ruangwa
tangu 2010, amezaliwa tarehe 22 December 1960 amesoma shule ya msingi mnacho mwaka 1970 hadi 1976 ,na baadaye
kujiunga elimu ya Sekondari shule ya Sekondari Kigonsera mwaka 1977 hadi 1980
mwaka 1991 alijiunga na chuo cha ualimu
Mtwara hadi 1993 ambapo alihitimu na kujiunga na chuo kikuu cha Dar es Salaam 1994 hadi 1998.
Mwaka 1999 alikwenda chuo kikuu
cha Storcklm.
Mbali na kuwa mbunge pia amewahi kuhudumu kama mkuu wa wilaya
mwaka 2006 hadi 2010, katibu chama cha walimu wilaya na mkoa na mwalimu.
Rais Dakta JOHN POMBE MAGUFULI leo asubuhi alipeleka Bungeni jina la Mbunge
huyo wa Ruangwa,MAJALIWA KASIM MAJALIWA ili liidhibishwe na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kuwa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baada ya jina lake kupendekezwa
Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Jaji GEORGE MASAJU aliwasilisha hoja kwa wabunge
juu ya uteuzi huo.
Wabunge waliopata nafasi ya
kuchangia kuunga mkono hoja hiyo ya
Mwanassheria Mkuu, wamemuelezea MAJALIWA kuwa ni mtendaji mzuri wa shughuli za
Serikali na kwamba atafaa kumsaidia Rais MAGUFULI.
Wakati huo huo Dokta Tulia Ackoni
Mwansansu amechanguliwa na wabunge kuwa naibu spika wa bunge baada ya kupata
kura 250 sawa na asilimia 71.2 baada ya kuchuana vikali katika nafasi hiyo na
mbunge kutka CUF Mh.Magdalena Sayaka aliyepata kura 101 sawa na asilima 28.8.
Baada ya uchaguzi huo Mh.Mwanasasu
aliapishwa na Spika wa Bunge Mh.Job Ndugai ili kumpa fursa ya kuanza kutekeleza
majukumu yake kama Naibu Spika wa Bunge.
Wakati huo huo waliokuwa wagombea
katika nafasi ya Naibu Spika wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka CCM Dr.Tulia
Akson Mwansasu na Bi.Magdalena Sakaya CUF/Kwa Mwavuli wa UKAWA waliokuwa
wanachuana nafasi hiyo.
0 comments:
Post a Comment