Image
Image

Mchakato wa kumpata Spika wa Bunge,Rungwe aingia Mitini.


Mgombea wa nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Hashim Rungwe ameshindwa kuonekana Bungeni mjini Dodoma wakati wa mchakato wa kujinadi kwa wabunge na kuchaguliwa kuwa Spika wa Tanzania.

Akizungumza bungeni hapo Katibu wa Bunge Dr.Thomas Kashilila  wakati wa kutaja majina ya wagombea wa nafasi hiyo amesema kuwa hadi asubuhi ya leo hakupata taarifa yeyote ya kuto kufika Bungeni hapo kwa Mh.Rungwe Spunda.

Licha ya kutofika kwa Mh.Rungwe bado zoezi la kumpata Spika liliendeshwa na mwenyekiti wa muda Mh.Andrew chenge kwa kila mgombea kunadi sera zake mbele ya wabunge wateule ili kuweza kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo nyeti katika bunge la 11 la Tanzania ambalo linatengeneza historia Mpya.

Hata hivyo baada ya kila mgombea kupewa nafasi ya kujinadi mbele ya wagombea wateule kwa kila mmoja kupewa dakika tatu za kujieleza kwa kila mmoja kwa nafasi yake aliahidi kuendesha bunge la kitofauti tofauti na mabunge yote yalio pita.

Wamesema katika Bunge hili la 11 ambalo linaonekana linachangamoto nyingi watahakikisha kuwa kwa nafasi watakayopewa kwa kuchaguliwa watahakikisha kuwa bunge linafuata mingi na kanuni na hivyo kuweka mbele maslahi ya taifa na vyama baadae ili kuweza kujenga taifa moja lisilokuwa na ubaguzi wa kupendelea chama chochote ndani ya Bunge.

Wagombea ambao waliomba nafasi hiyo ya juu ya Uspika wa Bunge la Tanzania walikuwa nane na walioomba ridhaa ya kupigiwa kura bungeni walijitokeza 7 huku mgombea wa nane akiwa hayupo lakini bado ananafasi kubwa ya wagombea hao kumpigia kura.

Waliokuwa teuliwa kuchuana kwenye nafasi hiyo ya uspika kutoka katika vyama vyao baada ya kupitishwa.-Peter Sarungi (AFP) -Hassan Kisabiya (N.R.A) -Dkt Godfrey Malisa(CCK) -Job Ndugai (CCM), -Goodluck Ole Medeye (CHADEMA) -Richard Lymo (T.L.P) -Hashimu Rungwe(CHAUMA) -Robert Kisinini (DP).

Kwa sasa zoezi linaloendelea huko bungeni ni kuhesabu kura zilizopigwa na wabunge wateule kuchagua Spika kati ya wagombea hao 8.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment