Image
Image

Polisi Mkoani Mbeya yanasa raia watatu wa china wakiwa na pembe 11 za Faru.


Watu watatu raia wa china wanashikiliwa na jeshi la Polisi mkoani Mbeya kwa tuhuma za kukamatwa na pembe 11 za faru wakijaribu kuziingiza nchini wakitokea nchi jirani ya Malawi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, kamishana msaidizi mwandamizi wa Polisi,Ahamed Msangi amesema watuhumiwa hao ambao wote ni raia wa china,wamekatwa katika mpaka wa Tanzania na Malawi wa Kasumulu wilayani Kyela wakati wakijaribu kungia nchini kwa gari aina ya TOYOTA HILUX.

Aidha Kamada Msangi amesema kuwa gari hilo baada ya kukaguliwa ndipo likagundulika kubeba nyara za serikali ambazo ni pembe 11 za faru walizozificha chini ya CHASES ya gari hilo. 

Maofisa wa idara za uhamiaji na mamlaka ya mapato Tanzania TRA, ambao pia wameshiriki katika zoezi la kuwatia mbaroni wachina hao, wamesema kuwa licha ya wachina hao kuwa na Pasport zinazowaruhusu kuingia nchini kihalali,lakini ni kosa kuingia na vitu ambavyo vimezuiwa,hivyo kwa kufanya kosa hilo wanaweza kuchukuliwa hatua za Kisheria.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment