Image
Image

Tume ya haki za binaadamu Zanzibar yatoa msimamo wa mgogoro wa urais Visiwani humo.



Tume ya haki za binaadamu  na utawala bora imetoa msimamo wa  mgogoro wa urais wa Zanzibar na kusema haina mamlaka ya kisheria  ya kutoa  tafsiri ya kisheria  kuhusu  vipengele  vya katiba kuhusu uongozi wa urais wa Zanzibar.

Msimamo huo umetolewa na Mwenyekiti  wa tume hiyo nchini  Bw.Tom Bahame Nyanduga wakati akiongea na waandishi wa habari kutoa amaelezo ya ziara ya tume kisiwani Zanzibar ambapo imekuja kufuatilia hali ya mvutano wa Mgogoro wa uchaguzi wa Zanzibar  ambapo amesmema suala la rais wa Zanzibar kuendelea kuwepo madarakani  hilo si la tume na wenye mamlaka ya kutoa tafsiri ya katiba kuhusu kipengele hicho ni mahakama kuu na siyo tume.

Akizungumzia uchaguzi mkuu wa Zanzibar na mwenyekiti huyo wa tume amesema kumeonekana kuwa kila chaguzi za Zanzibar kunakuwepo na matatizo na kuibuka migogoro  ambayo ikaichiwa husababisha uvunjanji wa haki za binaadaamu hivyo tume yake iangalia uwezekano wa kushauri njia sahihi za kundoa kasoro hioz kwa muda mfupi na mrefu.

Tume ya haki za bindaamu na utawala bora ni taasisi ya kwanza ya muungnao kuja Zanibar  mara baada ya kufutwa kwa uchagzui mkuu wa Zanzibar ambapo ikiwepo hapa itakutana na wadau wa sekta hiyo wakiwemo makamishna wa tume na vyama vya siasa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment