Wakizungumza
na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam kwa niaba ya mganga mkuu wa mkoa wa
Dar es Salaam,Bi.Victoria Bura amesema ugonjwa wa kipindupindu imeathiri mikoa
mbalimbali ikiwemo mkoa wa Dar es Salaam ambapo watu 53 wamepoteza maisha
kutokana na ugonjwa huo huku watu 4076 wakidaiwa kuugua ugonjwa huo laktika
wilaya tatu za jiji la Dar es Salaam lakini kwa sasa hali imekuwa nzuri huku
mkuu wa kitengo cha elimu ya afya kwa umma kutoka wizara ya afya na usyawi wa
jamii akieleza juhudi walizofanya katika kuelimisha jamii na kupata matokeo
mazuri hadi sasa kwa nchi nzima.
Dakta
Mery Kitambi kutoka kitengo cha dharura na maafa kutoka wizara ya afya na
ustawi wa jamii,amsema watu 106 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huo huku
watu 7598 wakidaiwa kuugua ugonjwa huo katika mikoa 17 na wilaya 39 ambazo
ugonjwa huo ulifika jitihada nyingi zimefanyika kupambana na ugonjwa huo hivyo
wadau wotee wametakiwa kushirikina na wizara ya afya katika kupambana na
ugonjwa huo kwa maslahi ya taifa huku halmshauri ya kinondoni nayo ikionekana
kuathirika na ugonjwa huo.
0 comments:
Post a Comment