Image
Image

UTAFITI:Asilimia 80% ya waandishi wa habari hawana mikataba.

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) uliolenga kuangalia hali ya vyombo vya habari nchini umebaini kuwa asilimia 80 ya waandishi wa habari ambao wanafanya kazi katika vyombo mbalimbali Tanzania hawana mikataba.
Akiongea wakati akitoa ripoti ya utafiti huo mwenyekiti wa MISA, Bw. Simon Berege amesema kuwa kutokana na waandishi wa Habari kutokuwa na mikataba ya kudumu inawawia vigumu kuanzisha vyama ambavyo vitazungumza badala yao hali inayopelekea hata kuwepo sheria ambazo zinakandamiza uhuru wa vyombo vya habari nchini.
Bw. Berege ameongeza kuwa utafiti huo pia umebaini kuwa kuwepo kwa sheria zinazokandamiza uhuru wa vyombo vya habari nchini kunainyima jamii fursa ya kupata taarifa muhimu ambazo zingeweza kuwa chachu ya maendeleo nchini.
Kwa upande mwingine serikali imeombwa kuweka uwiano wa utoaji matangazo ya biashara baina ya vyombo vya umma na vile vinavyomilikiwa na watu binafsi nchini, ili kuviwezesha vyombo binafsi navyo kuimarika kiuchumi na hatimaye viweze kutoa maslahi bora kwa watumishi wake.
Katibu Mtendaji wa Chama cha Wamiliki wa Habari nchini Bw. Henry Muhanika, ametoa ombi hilo leo muda mfupi baada ya hafla ya tathmini ya mwenendo wa vyombo vya habari nchini ambapo pamoja na mambo mengine, imebainika kuwa hali ya kiuchumi ya vyombo hivyo sio nzuri.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment