BASATA YAMLILIA BI KIDUDE
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa
msanii nguli wa tasnia ya muziki wa taarab nchini Bi Kidude.
Baraza limestushwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa ya kifo hiki cha Bi
Kidude ambaye mchango wake katika muziki wa taraab ni mkubwa mno na unahitajika sana, pengo aliloliacha ni kubwa kwani ubunifu wake bado unahitajika katika tasnia hii.
Baraza linatoa pole kwaamilia ya marehemu na wasanii wote nchini, aidha tunawatakia moyo wa subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na mpendwa wetu.
Mwenyezi Mungu aipumzishe mahala pema peponi roho ya marehemu. Baraza liko pamoja na
familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Imetolewa
na
Godfrey
Mngereza
Kaimu
Katibu Mtendaji
Baraza
la Sanaa la taifa.
0 comments:
Post a Comment