BENKI ya Wanawake Nchini(TWB)imekuwa jipu kutokana
na kutokuwa na msaada wa kuwaendeleza wanawake ili waweze kunyanyuka kiuchumi.
Hayo ameyasema leo Waziri wa Afya,Maendeleo Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati kilele cha siku ya wanawake Duniani ambayo huadhimishwa kila Machi 8 katika mwaka,amesema kuwa benki ya TWB haijatengeneza mazingira rafiki kwa wanawake ili waweze kuitumia.
Amesema kuwa benki zingine zimeweza kufanya kazi za kuwainua wanawake kwa kuwapa mikopo lakini benki ya TWB haifanyi hivyo huku wakijua na wajibu wa kufanya hivyo.
Ummy amesema licha ya changa oto ya mikopo kuna baadhi ya Halmashauri hazitoi asilimia tano katika mfuko wa wanawake katika kuwaendeleza kiuchumi
Ummy amesema wanawake wanatakiwa kufika asilimia 50 katiki kuweza kwenda sambamba na wanawake lazma waonyeshe uwezo na fursa mbalimbali za uchumi kuzitumia.
Amesema wanawake wakipata nafasi ni sawa na kuwa na jamii nzima yenye mafanikio ya mwanamke mmoja hivyo kila mwanamke afanye kazi kwa kujituma katika nafasi yake iwe ya kiuchumi ,kutoa huduma kwa jamii.
Aidha amesema kuwa kila wanawake 10 ,wanawake sita (6) wanamaambukizi vya virusi ukimwi na kila wanaume 10 wanne (4) wanaambukizi ya virusi vya ukimwi.
Waziri wa Afya amesema kutokana na takwimu hizo lazima licha ya kuwakamata wanawake wanaojiuza ‘makahaba’ kunahitaji na kuwakamata wanaume ambao wanafanya mchezo huo katika kupunguza maambukizi kwa wanawake.
Katika Maadhimisho hayo mbunge wa Njombe Kusini, Edward Mwalongo amepata tuzo kupaza sauti katika bunge juu ya mtoto wa kike kupewa dhana ya kujikinga wakati wa hedhi ili aweze kusoma.
Waziri Ummy ameipongeza Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kwa kuendelea kuelimisha wanawake juu ya vipodozi feki pamoja na vyakula kutokana na kutambua wajibu kulinda wanawake.

0 comments:
Post a Comment