Makamu wa Rais Dk.Mohammed Gharib Bilal amewataka Waislamu kutambua umuhimu wa kudumisha amani umoja na mshikamano wa watanzania na kuwaonya baadhi ya watu au kikundi cha watu wanaotaka kutumia dini hiyo kuvunja amani ya nchi.
![]() |
| Dk.Mohammed Gharib Bilal - Makamu wa Rais Tanzania. |
Amesema utunzaji wa amani ya nchi ni pamoja kuvumiliana na kuheshimiana baina ya watu wa imani ya dini moja dhidi ya nyingine na kwamba kwa kufanya hivyo watakuwa wameenzi mafundisho ya Mtume Muhammed SAW.
![]() |
| Jumanne Maghembe - Waziri wa Maji Tanzania. |
Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na Katibu Mkuu wa Taasisi ya Masheikh na wanazuoni Tanzania Sheikh Khamis Mataka wamehimiza umoja na mshikamano miongoni mwa waislamu pamoja na umuhimu wa kutii na kufuata sheria za nchi.

.jpg)

0 comments:
Post a Comment