Katika
hali ya kawaida watu wengi wamezoea kusikia na kuambiwa kuwa Chocolate
si kitu kizuri na kuna sababu nyingi za kukufanya uamini kuwa chocolate
si nzuri.
Watu
husema inaharibu meno, wengine hudai kuwa inasababisha kisukari na
wengine huenda mbali zaidi wakidhani kuwa inaharibu ngozi kutokana na
wingi wa mafuta iliyo nayo.
Watoto wadogo ambao wamezoeleka kuwa wapenzi wakubwa wa chocolate ndio huvunjwa moyo na wazazi/walezi wao katika hili.
Ukweli
ni kwamba Chocolate si mbaya kwa afya yako na hii inatokana na matokeo
ya utafiti rasmi (research) ambayo yamekuja na faida hizi nne ambazo
zitakufanya ule chocolate mara nyingi zaidi uwezavyo.
1.Chocolate ni nzuri kwa Moyo wako.
Utafiti
unaonyesha kuwa chocolate inaweza kusaidia kupunguza magonjwa ya moyo
na hata shinikizo la damu na shambulio la moyo (Heart Attack).
Chocolate
nyeusi zimethibitika kuwa na uwezo wa kusaidia moyo ambao umeanza
kuathirika na matatizo ambayo yanaweza kukuletea ugonjwa wa kiungo hicho
muhimu kwenye mwili wa binadamu.
2.Inapunguza kisukari.
Ni vigumu kuamini lakini ukweli halisi ni kwamba , chocolate inasaidia kuondoa uwezekana wa mtu kupata kisukari.
Watu
ambao wamekuwa na kawaida ya kula chocolate walau kipande kidogo mara
moja kwa siku kwa muda wa siku tano wanakuwa na uwezo wa kuwa na kinga
dhidi ya kisukari kuliko wale ambao hawali chocolate kabisa.
3.Kupambana dhidi ya Msongo wa mawazo (stress).
Tafiti za kisayansi zimethibitisha kuwa chocolate inasaidia kupunguza msongo wa mawazo au stress.
Watu
wenye msongo wa mawazo hushauriwa kula walau gramu 45 za Chocolate
kila siku wa muda wa wiki mbili ili kushusha msongo wa mawazo.
Chocolate hushusha kiwango cha Homoni ya Cortisol mwilini, homoni hii huongeza au kupunguza msongo wa mawazo.
4.Chocolate husaidia kujikinga dhidi ya Jua.
Chocolate husaidia ngozi ya mawadamu kujikinga dhidi ya madhara ya miale ya jua.
5. Imesemekana kuwa Watu wanaokula Chocolate mara kwa mara huwa wembamba. Hii ni kwa
mujibu wa utafiti mpya. Karibu watu 1000 nchini Marekani walifanyiwa
utafiti ambao wamekuwa makini katika vyakula vyao. Waliokuwa wakila Chocolate mara kwa mara
walipatikana wakiwa wembamba kuliko wenzao ambao hula Chocolate baada ya
muda.
Wanasayansi wanasema, japo Chocolate ina sukari nyingi, ina viungo
ambavyo husaidia kupunguza uzito wa mwili, lakini siyo kuchoma mafuta.
Flavonoids
ambazo zinatumika kutengeneza chocolate zina chembechembe ya vimelea
(microorganisms) vinavyoweza kusaidia ngozi na kuikinga dhidi ya miale
ya jua
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Shukran kwa makala imetulia
ReplyDeleteMakala nzuri
ReplyDelete