Magonjwa ya kurithi ni yapi?
Haya
ni magonjwa ambayo yapo kwenye koo za watu fulani na hurithiwa kutoka
kizazi mpaka kizazi lakini pia magonjwa haya huweza kutoka kwa mwanamke
na mwanaume ambao kwa macho ni wazima kabisa na kuzaa watoto wenye matatizo ya kiafya.
Kwenye
jamii zetu za kiafrika ni jambo la kawaida sana kuzaa tu bila kupima
kujua kama kuna hatari ya kuzaa mtoto mwenye matatizo makubwa ya kiafya
kutokana na vimelea vya kurithi yaani DNA ambazo wazazi husika
wamezibeba, mimba nyingi zimekua zikisingiziwa kwamba hazikupangwa na
wakati kila mtu anajua mwisho wa ngono zembe bila njia yeyote ya uzazi
wa mpango ni mimba.
Hii ni tofauti na nchi zilizoendelea ambapo
wazazi hupima vipimo hivi kabla ya kuamua kuzaa na hata ikigundulika
mtoto anayekuja atakua na matatizo mimba hiyo hutolewa ili kuepusha
maumivu ambayo mtoto huyo angeyapata kama angezaliwa na maumivu ya
kisaikolojia na kiuchumi ambayo wazazi wanaozaa watoto kama hawa
wanayapata, hii ni kwasababu ya kulazwa mara kwa mara kwa mtoto husika
na kushindwa kufanya kazi maisha yake yote.
Hivyo nchi zilizoendelea
watoto wanaozaliwa na magonjwa ya kurithi wametokomezwa kwa kiwango
kikubwa sana tofauti na afrika ambapo watoto hawa ni wengi sana na kila
siku wanazidi kuzaliwa, wakati wangeweza kuzuilika kama sisi wahusika na
serikali ingechukua hatua kukomesha hili kwa kuingiza vifaa vya
kitaalamu ya kuyagundua magonjwa haya muhimu.
Ni kweli vipimo vingi
havipatikani hasa maeneo ya vijijini na hata mijini lakini kuna watu
ambao wako kwenye nafasi kubwa ya kuzuia na kupunguza idadi ya watoto
hawa wanazaliwa kila siku, hasa watu wanaoishi mijini na wenye uwezo
kifedha lakini hata wewe ambaye huwezi kupata vipimo hivi hebu jaribu
kwenda ukweni kwa mumeo au mkeo unaweza ukaona ugonjwa wa kurithi ambao
sio wa kawaida huko na kufanya maamuzi vizuri au unaweza ukamuuliza
mumeo au mkeo ili awe muwazi kabla ya kufunga ndoa kwani magonjwa
mengine yanaonekana kwa macho tu.
Magonjwa haya ni kama yafuatayo
1. Sickle cell disease;{siko seli]
Huu
ni ugonjwa wa kurithi ambao mtoto hurithi kutoka kwa baba na mama
ambapo wazazi wawili ambao wanakua hawana dalili yeyote hubeba ugonjwa
huu kwenye damu zao yaani carrier na wanakua na uwezekano wa 25% ya kumzaa mtoto
huyu ambae ataugua na kua na dalili zote za ugonjwa huu. Ugonjwa huu ni
hatari sana. Mwaka 2013 ugonjwa huu uliua watu laki mmoja na elfu
sabini na sita duniani kote wengi wakitokea Africa hasa chini ya jangwa
la sahara. Watoto hawa huanza na dalili za kuvimba vidole wakiwa na umri
wa miezi mitatu, kuvimba vichwa, kua na miguu na mikono mirefu na
miembamba, kulalamika maumivu makali, kuishiwa damu sana na kadhalika
ukubwani.
Kama wapenzi wakipimwa wakakutwa wote wameubeba ugonjwa huu
kwenye damu zao yaani carriers ni vizuri wakaairisha ndoa hiyo kwani
watakaribisha matatizo makubwa kwenye maisha yao. Kama unataka kujua
umebeba ugonjwa huu ukienda hospitali kubwa za rufaa wana uwezo wa
kuwapima na kujua. Ugonjwa huu pia unaweza kupimwa kwa kuchukua maji
kwenye tumbo la mama kabla hajazaliwa hivyo kuamua kuendelea na mimba au
kuitoa. Japokua kutoa ni kosa kisheria nchini Tanzania.
Watoto hawa huishi kwa mateso makali na 50% watakufa kabla ya miaka 40 kwa nchini kwetu Tanzania hakuna
data kamili za watu hawa lakini wasichana wengi wenye ugonjwa huu hufa
wanapoanza kuziona siku zao kwani damu hupungua zaidi na viungo vingi
kushindwa kazi.
2. Haemolytic diseases of the new born;
kuna aina
kuu nne za group za damu yaani A, B, AB, na O ambazo group hizo mtu
anaweza kua positive au negative mfano mtu mwingine anaweza kua A
positive na mwingine akawa A negative au B positive na mwingine B
negative.Sasa swala ni kwamba watu wa negative wakioana hakuana shida au
watu wa positive wakioana hakuna shida LAKINI mwanaume wa positive
akioa mwanamke wa negative mtoto wa kwanza atazaliwa vizuri lakini
ataacha vitu vinaitwa antibodies ambavyo kazi yake itakua ni kuharibu
mimba zote zitakazofuata kutoka kwa mwanaume huyu. Kipimo hichi ni rahisi sana na kinapatikanakaribia
hospitali zote Tanzania na hata kama mmeshaoana tayari na mna tatizo
hili kuna dawa maalumu inaitwa RHoGAM mama mjamzito anachomwa wiki ya 28
mpaka 32 kuzuia vifo hivyo.
3. Albinism{Ualbino]:
Huu ni ugonjwa
wa kurithi ambao motto huzaliwa bila vimelea vya melanin au kua na
uchache wa vimelea hivyo ambavyo humfanya mtu apate rangi ya ngozi yake.
Mara nyingi wazazi wote wawili wa mtoto huyu hubeba ugonjwa huu kwenye
miili yao bila kua na dalili yeyote na wao kumzaa mtoto ambaye ni albino
lakini pia kuna aina za ualbino ambazo mzazi mmoja anaweza kusababisha
albino kuzaliwa bila mama kua na vimelea vya ualibino.Mtoto huyu
huzaliwa akiwa na matatizo ya kutoona vizuri na makengeza, ngozi na
nywele nyeupe sana. Kua albino sio ugonjwa lakini watu hawa hua kwenye
hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa kansa ya ngozi. Sio rahisi kupima
kujua kama mtu anabeba vimelea vya ualbino kwenye mwili wake lakini
inawezekana kupima mtoto aliyeko tumboni na kugundua kama nia albino au
sio kwa nchi zilizoendelea au unaweza kumjua mwenzako kwa kuona albino
kadhaa kwenye ukoo wao.
4. Magonjwa ya akili:
katika jamii kuna
watu hua wanafanya vitu ambavyo sio vya kawaida mpaka unajiuliza huyu
mtu amechanganyikiwa au vipi..yaani ni mtu wa fujo, hajifunzi kwa makosa
ya nyuma, unasikia mtu kamuua mzazi wake,anavunja sheria mara
kwa mara, kunywa pombe sana, anakasirishwa na vitu vidogo sana au
maisha yake ya mahusiano yanakua ni ya ugomvi kila siku yaani kwa kifupi
anakua tofauti na wengine. Dalili hizi sio za kupuuzia kuna
uwezekano mkubwa sana wa kuzaa watoto wa aina hii ambao huanza kusumbua
tangu wakiwa shule ya msingi na kupata matatizo makubwa ukubwani. Shida
hizi hazihitaji vipimo ni wewe kutoa maamuzi mapema kabla hamjaamua
kuzaa naye kwani mambo hayo yanarithiwa na mimi nimeshashuhudia familia
nzima ya watu waliokua hawana akili nzuri yaani walikua wehu kabisa.
5. Magonjwa ya kansa;
Ugonjwa wa kansa
haurithiwi lakini kuna baadhi ya koo zina vimelea{genes] ambazo baadae
husababisha kansa. Ni vizuri kujua vyanzo vya vifo vya ndugu wa mwenza
wako kabla ya kuamua kuzaa naye kwani ugonjwa huu unaweza kua ni mbaya
zaidi kuliko magonjwa yote ya kurithi. Kuna familia naifahamu nyumba
ilifungwa kwani watu wote waliuawa na kansa yaani mume na watoto wote
waliozaliwa, dada na kaka wote wa mume isipokua mke tu aliyekua ameolewa
pale.
6. Ugonjwa wa kisukari;
Ugonjwa huu yaani
diabetes mellitus type 2 unawapata sana wagonjwa watu wengia ambao kwao
kuna ugonjwa huu. Yaani kama baba yako na mama yako wana kisukari
uwezekano wa wewe kupata kisukari ni asilimia hamsini. Maana yangu ni
kwamba ukioa au ukiolewa na mtu ambao kwao kuna wagonjwa wa kisukari
ujue kuna uwezekano wa mtoto wenu mmoja kuugua ugonjwa huo miaka ya
baadae. Hivyo hua tunashauri kama wazazi wako wana kisukari kuepuka kua
mnene kwani utakikaribisha mapema.
7. Ugonjwa wa asthma au pumu;
Ugonjwa
huu ambao hushambulia mfumo wa upumuaji hufuata sana ukoo fulani wa
watu japokua pumu zipo za aina mbili ile ya kurithiwa na ile ambayo sio
ya kurithiwa hivyo kama ukoo unaoenda kuoa au kuolewa una wagonjwa
wawili au watatu wa asthma kuna uwezekano mkubwa sana wa kumzaa mtoto
mwenye pumu baadae, ugonjwa ambao huua haraka kama usipopata ufuatiliaji
wa kutosha
8. Ugonjwa wa kifafa;
Japokua ugonjwa hu huweza
kusababishwa na magonjwa mengine kama homa ya uti wa mgongo, ulaji wa
nyama ya nguruwe na kadhalika ugonjwa huu umeonekana kufuata
koo Fulani za watu yaani kama unaenda kuoa kwenye ukoo ambao unafahamu
kuna wagonjwa wa kifafa uwezekano wa kuzaa watoto wenye kifafa upo hivyo ni vema kuingia unajua.
9. Umbilikimo:
Huu
ni ugonjwa wa kurithi ambao watu wanazaliwa sana kitaalamu unaitwa
achondroplasia, wazazi wa watoto hawa ambao hua na mikino na miguu
mifupi sana huweza kua kawaida kabisa lakini kutokana na kurithi vimelea
vya ugonjwa huu hujikuta wanamzaa mtoto huyu na mtoto huyu baada ya
muda Fulani akioa anazaa mtoto wa hivi hivi kwani mzazi mmoja tu huweza kusababisha hali hii.
10. Magonjwa ya upofu;
Kuna
koo ambazo watoto huzaliwa na vimelea vya hali ambayo husababisha upofu
baadae au ikasababisha upofu hata kabla ya mtoto kufikisha miaka
mitano. Mtoto huzaliwa na mtoto wa jicho kitaalamu kama congenital
cataract ambayo huziba jicho taratibu na baadae mtu hataona kabisa na
unaweza ukakuta ukoo una vipofu wengi na chanzo husika hakifahamiki.
Mwisho:
Haya
ni baadhi ya magonjwa ambayo labda yameathiri watu wengi kwenye jamii
zetu lakini yapo mengine mengi ambayo siwezi kuyataja na makala hii
haijaandikwa kuwatenga au kuwasema vibaya watu wenye matatizo haya
kwamba wasioe au wasiolewe lakini ni kujaribu kuongea ukweli na kuepusha
watu wenye tatizo moja kuzaa mtoto kwani ni kujiongezea matatizo tu kama nilivyosema hapo mwanzoni na kuleta viumbe ambavyo vinakuja duniani kuteseka sana.
Ni
bora waendelee kuzaliwa carriers yaani wanaobeba vimelea bila kuugua
kuliko kuendelea kuwazaa wagonjwa.hivyo kama wewe unajua kwenu kuna
shida fulani ni bora kuzaa na mtu ambaye kwao hamna shida kabisa kwani
ukizaa na mtu mwenye matatizo kwao pia ni hatari zaidi na kama ukiamua
kukaidi na kuzaa hivyohivyo uzae unajua kwamba haya magonjwa yapo. niwape pole ambao tayari ni wagonjwa wa hali hizi na wale wenye ndugu wenye hali hizi.dunia inatambua maumivu yenu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment