Serikali
ya Kenya imefichua kwamba imewakamata raia wanane wa Tanzania waliokuwa
katika harakati za kujiunga na kundi la wapiganaji la al-Shabab nchini Somalia.
Katika taarifa iliotumwa
katika vyombo vya habari, polisi wanasema raia hao waliokamatwa katika
kipindi cha miezi miwili iliopita walikiri kuwa mbioni kujiunga na kundi
hilo la ugaidi.
Hatua hiyo inajiri siku chache baada ya kundi la watu wanaojidai kuwa wapiganaji wa Kiislamu kuweka video mtandaoni likidai uwepo wa wapiganaji wa Kiislamu nchini Tanzania
Video hiyo iliwaonyesha wanaume hao wakiwa wamejifunika nyuso zao kwa vitambaa na barakoa.
Wanadai wamo katika mji wa Tanga na kuwahimiza Waislamu katika taifa hilo la Afrika Mashariki kujiunga na kampeni yao.
Wapiganaji wa Kiislamu wadai 'wamo Tanzania'
Polisi wa Kenya pia wanasema wamefanikiwa kutibua njama ya wanachama wa kundi linalojiita Islamic State ya kutekeleza mashambulio nchini humo na kuwakamata washukiwa wawili.
Wawili
hao Kiguzo Mwangolo Mgutu na Abubakar Jillo Mohammed walipewa mafunzo
ya kuwa na itikadi kali kabla ya kuingizwa katika kundi la IS na
Mohammed Ali aliyekamatwa awali na ambaye anasaidia polisi na uchunguzi,
polisi wamesema.
Kulingana na taarifa hiyo, kufuatia kukamatwa kwa
Mohammed Ali, wafuasi wake wamekuwa wakipanga kufanya mashambulizi ya
kulipiza kisasi sana wakilenga sekta ya uchukuzi wa abiria.
Kukamatwa kwa wawili hao, kumezuia kutokea kwa mashambulio katika miji ya Nairobi na Mombasa.Source:BBC.
Home
Kimataifa
Slider
Kenya yawanasa raia wanane wa Tanzania waliokuwa katika harakati za kujiunga na al-Shabab.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment