Image
Image

EXCLUSIVE: CAG AIBUA ULAJI FEDHA ZA SERIKALI.



Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ameibua ulaji wa kutisha wa fedha za serikali unaohusisha kulipa mishahara zaidi ya mara moja, kuchakachua tarehe za kuzaliwa na kutorejesha masurufu.
Ripoti hiyo iliwasilishwa juzi bungeni na CAG, Ludovick Utouh na kuibua ulaji wa kutisha wa fedha za umma.

Ripoti  hiyo libainisha kuwa  zaidi ya Sh. bilioni 1.9 za masurufu yaliyotolewa kwa wafanyakazi wa halmashauri, nyingi hayajarejeshwa na kwamba kuanzia mwaka 2008 hadi 2012 fedha za masurufu yaliyotolewa kwa wafanyakazi wa halmashauri yaliyotakiwa kurejeshwa hazijaonekana hadi sasa.
Mdhibiti amebainisha  kuwa katika mwaka wa fedha wa 2011/12 karibu Sh. milioni 700 zimetumika kulipa mishahara ya marehemu, wastaafu, walioachishwa ama kuacha kazi katika halmashauri 43.
Ludovick Utouh -  Mdhibiti  na Mkaguzi Kuu Hesabu za Serikali.
Ofisi ya Mdhibiti ilibaini kuwa malipo ya mishahara katika halmashauri mbili yalionyesha kuwa mwaka wa fedha 2011/12 wafanyakazi 10 walikuwa na namba tofauti za utumishi hivyo kuleta hofu ya kutengewa fedha zaidi za mishahara.

Ripoti hiyo  ilisema watumishi sita ni wa Halmashauri ya Rungwe na wanne ni wa Namtumbo waolikuwa na namba za watumishi zaidi ya mmoja . Ilionya kuwa mtumishi kulipwa mishahara mara mbili ni matumizi mabaya ya fedha za umma.

Ripoti ya Mdhibiti ilibaini kuwa Halmashauri 13 zina wastaafu 198 ambao hawajafutwa kwenye orodha ya mishahara Hazina hivyo licha ya kula pensheni wanaendelea kulipwa.
Kati ya wilaya hizo inayoongoza ni Newala yenye wastaafu 60, ikifuatiwa na Manyoni 26, Singida 21 na Morogoro 19 na ya mwisho ni Ngara yenye waastaafu watatu.

Ilionya kuwa kuchelewa kufuta wastaafu hao kwenye orodha ya malipo kunasababisha kulipa wafanyakazi hewa.

Ripoti imegundua kuwa watumishi 1, 531 hawana tarehe sahihi za kuzaliwa .
“Ilibainika kuwa halmashauri zimeonyesha tarehe za kuzaliwa za watumishi 1,531 zisizosahihi zilizoingizwa kwenye mfumo wa malipo zikitaja tarehe za kuzaliwa kuwa ama 1.1.1700, au 1.1.1900 na 1.1.2012 ambazo pia zimepelekwa kwenye rejista kuu ya malipo ya Hazina.”

Halmashauri zilizokuwa na tarehe feki ni 15 na iliyoongoza kuchakachua tarehe hizo ni Musoma yenye watumishi 634, nyingine ni Serengeti wafanyakazi 363 , Ileje 197 zikifuatiwa na Mbeya, Rungwe, Moshi, Arusha na Mbarali.

Mdhibiti alisema : “Hii inamaanisha kuwa tarehe halisi za kustaafu za wahusika hazijulikani…hivyo zisiporekebishwa matatizo makubwa ya kifedha yanaweza kutokea wakati wa kulipwa mafao ya kustaafu.” Ripoti ilionya.

Karibu Sh. bilioni 1.06 zilizokatwa kwenye mishahara ya wafanyakazi hazikuwasilishwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii. Halmashauri zilizobainika ni saba zikiwamo Makete yenye zaidi ya Sh. milioni 604, Mbarali milioni 162 na Kilosa milioni 146 .

Ripoti ilisema wanasiasa wanaingilia ukusanyaji mapato na kusababisha kero kubwa katika ngazi za serikali za mitaa. Watuhumiwa ni baadhi ya madiwani kuwakataza wananchi kulipa kodi ili kupata umaarufu kisiasa.

Pia Serikali Kuu kuingilia ukusanyaji kodi mfano mwaka 2011 Wizara ya Miundombinu ilikataza halmashauri kukusanya kodi ya mabango ya Wakala wa Barabara (Tanroads) yaliyoko kwenye hifadhi za barabara.

Ripoti ya mdhibiti iliwasilishwa bungeni juzi lakini tofauti na miaka ya nyuma mwaka huu haikujadiliwa mbali na kuwekwa mezani na kugawiwa kwa wabunge na wadau wengine. Tuhuma za ubadhirifu zilizoibuliwa mwaka jana na mdhibiti ziliwaondoa madarakani mawaziri sita na manaibu wawili.







Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment