Wakati watu 36 wakiwa wamefariki dunia jijini Dar es salaam kwa kufukiwa na kifusi cha ghorofa 16 Katika mtaa wa Indira Ghadi jijini Dares Salaam, napo huko arusha imekuwa ni majonzi baada ya wachimba migodi 20 kufukiwa na kifusi cha mgodi huo katika eneo la Moshoro, Mjini Arusha leo.
Kufuatia kuporomoka kwa kifusi hicho inaelezwa kuwa maiti za watu 14 ndiyo zilikuwa zimeopoelewa huku watu wawili tu ndiyo walikuwa wametoka wakiwa hai na kukimbizwa katika Hospitali ya Mt Meru kwa ajili ya matibabu kutokana na kuvunjika miguu na sehemu mbali mbali za miili yao.
Katika harakati za kuwaokoa na kunusuru maisha ya watu waliofukiwa katika kifusi hicho waokoaji walifanikiwa kuwaokoa watu wawili wakiwa hai ambao walitambuliwa kuwa ni Matei
Nenano na Lushooki Laizer wote wakazi wa jijini Arusha.
Vikosi mbali mbali vya uokoaji kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Polisi vilikuwamo vikiwa vinashirikiana na wananchi wakitoa msaada wa kufukua kifusi hicho kwa ajili ya kutoa watu waliofunikwa.
Vikosi mbali mbali vya uokoaji kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Polisi vilikuwamo vikiwa vinashirikiana na wananchi wakitoa msaada wa kufukua kifusi hicho kwa ajili ya kutoa watu waliofunikwa.
Pia zipo maiti zilizoopolewa za mmiliki wa magari ya
kubeba kifusi hicho, Julius Peter, Alex Mariaki, Gerald Lutakata, Hassan
Hamis, Sauli Raphael, Bariki Revelian na Kababuu Ruafela.
Huku wengine wakiwa ni Mwenda Kiboliboli, Japhet Jivaline, Benard Masai, Gerald Jacob, Fredy Losileani, Julius Palangyo na mtu ambaye alijulikana kwa jina moja la Christopher ambazo zilikuwa zimefukiwa kwenye mgodi huo wa Moshomo.
Huku wengine wakiwa ni Mwenda Kiboliboli, Japhet Jivaline, Benard Masai, Gerald Jacob, Fredy Losileani, Julius Palangyo na mtu ambaye alijulikana kwa jina moja la Christopher ambazo zilikuwa zimefukiwa kwenye mgodi huo wa Moshomo.
![]() |
| Askari wa JWTZ nchini tanzani wakiwa wamebeba mwili mmoja kati ya waliyepoteza maisha katika machimbo ya Moramu yaliyopo Moshono Arusha. |
Watu walioshuhudia tukio na taarifa hizo kuthibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Hemed Kilonge walisema lilitokea jana saa 5.00 asubuhi wakati shughuli za uchimbaji zikiendelea.
Kamanda Kilonge alisema wakati wachimbaji hao
wakiwa ndani ya shimo wakiendelea na kuchimba ‘moramu’, ghafla gema
liliporomoka na kuwafunika.
Mashuhuda walioshuhudia kadhia hiyo walisema wachimbaji hao walikuwa
wakifanya shughuli zao huku mvua kubwa ikawainanyesha huku wakiwa na wasiwasi kuwa huenda mvua hiyo ndio iliyosababisha kuporomoka kwa kifusi hicho na kusababisha watu kupoteza maisha.
Aidha kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo yeye lilazimika
kusitisha safari yake mkoani Tanga baada ya kupata taarifa ya tukio
hilo na baadaye alitangaza kwamba Serikali imeamua kufunga machimbo yote
ya `moramu’ hadi pale itakapotoa tamko lingine ili kunusuru maisha yawengine ikizingatwa na mvua zinazonyesha mkoani humo kwa sasa.
Mulongo yeye amesema kuwa ameguswa na tukio hilo lililosababisha vijana wengi kupoteza maisha ikizingatiwa vijana ni nguvu kazi ya taifa, hivyo ni suala la kuomba dua kwa mola kusudi atuepushie na mengine majanga yanayotokea bila kutegemea.
Kwaupande wa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema yeye amesema kuwa jambo hilo ni zito na linahuzunisha kwani hakuna mtu ambaye alikuwa anategemea kutokea kwa watu kufukiwa na kifusi huku akiitaka seikali Serikali kuweka kuhakikisha inaweka utaratibu wa kukabiliana na matukio ya aina hii pamoja na kuweka viashiria vya usalama katika maeneo ya machimbo mbali mbali nchini.
Kwa upande wake mbunge wa Arusha Mjini, Godbless
Lema aliitaka Serikali kuweka utaratibu wa kukabiliana na matukio ya
aina hiyo ikiwa ni pamoja na kuweka viashiria vya usalama maeneo ya
machimbo.


0 comments:
Post a Comment