Na. Mwandishi Wetu.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetakiwa
kupunguza watumishi katika baadhi ya tasisi za umma kutokanana na wengi
wao kutokuwa na taaluma kuhusu kazi walizopangiwa.
Kauli hiyo ilitolewa na mwakilishi wa jimbo la
Chake Chake Omar Ali Shehe wakati akichangia ripoti ya kamati ya katiba
na sheria ya baraza la wawakilishi kuhusu utekelezaji wa maagizo ya kazi
kwa Wizara ya Nchi Ofisi ya rais – Utumishi na Utawala bora mwaka
2012/2013…
Alisema katika utekelezaji wa mpango huo serikali
inaweza kushirikiana na wahisani watakaosaidia kulipa mafao ya
wafanyakazi watakaopunguzwa ili kupunguza wafanyakzi ambao ni mzigo kwa
serikali.
“Kwanini serikali iendelee kubeba mzigo mkubwa wa
wafanyakazi ambao hawana utalaamu. Ni vyema serikali ikawa na
wafanyakazi wenye taaluma na kazi wanazozifanya ili kuleta ufanisi,”
alisema Shehe ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ukaguzi wa mahesabu
(PAC).
Aidha mwakilishi huo aliungana na wajumbe wengine
katika baraza hilo kuiomba serikali kuongeza mishahara ya watumishi wa
umma katika bajet ijayo ya mwaka wa fedha 2013/2014 ili kuwawezesha
kumudu maisha yao.
Shehe and Mwakilishi wa Jimbo la Mjimkongwe kupitia
chama cha CUF Bw Ismail Jussa Ladu walisema uwezo wa serikali wa
kuongeza maslahi kwa wafanyikazi wao ni mkubwa hivyo ni vyema kuongeza
mishahaa inayolingana na gharama za maisha .
“Kwa uchache, mfanyakazi mwenye familia ndogo sana,
anatakiwa apate elfu 20 kwa siku, lakini inasikitisha kuwa serikali
inawalipa wafanyakazi wake chini ya elfu 10 kwa siku. Hali hii
inasababisha rushwa,” alisema Jussa.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakadiriwa kuwa
na watumishi zaidi ya 38 elfu nusu yao wanadaiwa hawana taluma za kazi
wanazozifanya.
Serikali ya Zanzibar inatakiwa kuchukuwa hatua
Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za
Serikali ya Zanzibar imeeleza changamoto kadhaa ambazo zinakabili ofisi
nyingi za umma ikiwa pamoja na kutofuatwa kwa sheria za fedha na
manunuzi.
Hayo amebainishwa na Ismail Jusa Ladhu katika
ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wakati akiwasilisha muhtasari wa ripoti
ya kamati ya kudumu ya katiba na sheria kuhusu utendaji katika baadhi
ya wizara za serikali kwa mwaka 2012/2013
Alisema serikali imekuwa ikichelewa kuchukuwa
hatua juu ya mambo yanayobainika katika ripoti za mdhibiti na mkaguzi
mkuu wa hesabu za Seikali mfano, uelewa ndogo wa wadau kuhusu ripoti za
mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za Serikali.
“Ni muhimu wadau, na wananchi kwa jumla
wakaelimishwa kuhusu ripoti za mkaguzi na kupewa fursa za kutoa maoni
yao kwa lengo la kuleta ufanisi,” alisema Jussa ambaye ni makamo
mwenyekiti wa kamati hiyo.
Jambo jengine ambalo serikali ni lazima ilifanyie
kazi ni kutokuwepo mashirikiano mazuri baina ya afisi hii (ya Mkaguzi)
na Wizara ya nchi (AR) utumishi wa umma na utawala bora na kusababisha
kupungua kwa ufanisi katika ofisi mbili hizo.
Jussa alisema “Yote hayo yamebainika baada ya
kamati ya katiba na sheria na utawala kutembelea katika ofisi hizo,
lakini pia kamati inashauri Serikali kuzichukulia hatua za kinidhamu
Wizara, Mashirika pamoja na tasisi zisizowasilisha hesabu zao za mwaka
kwa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali ikiwa na maelezo ya
ubabaishaji.”
Aidha Jussa kwa niaba ya kamati alisema kamati yake
inasisitiza agizo la kutaka mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali
kuimaisha utendaji na kufanya ukaguzi yakinifu na wa kina ili kuweka
wazi ubadhirifu katika taasisis za serikali bila woga.
Mwakilishi huyo alisema haipendezi kuona serikali
inakaa kimya bila kuchukuwa hatua baada ya kamati ya kuchunguza hesabu
kugundua matumizi mabaya na vyelelezo ambayo hayaonekani katika ripoti
ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali.
WAJANE na Mayatima Zanzibar wapigiwa Debe
Serikali ya zanzibar imeombwa kuwasaidia wajane na mayatima kisiwani Pemba ambao wanakabiliwa na matatizo mengi ya kimaisha.
Ombi hilo liliwasilishwa jana katika kikao cha
baraza la wawakilishi linaloendelea mjini hapa na mwakishi wa viti
maalum vya wanawake (CUF) Mwanajuma Faki Mdachi ambaye alimtaka waziri
kukutana na jumuia mpya ya wajane na watoto yatima pemba.
Akijadili ripoti ya utekelezaji wa kazi katika
wizara ya Ustawi wa jamii na maendeleo ya vijana, wanawake na watoto kwa
mwaka 2012/2013, Mwanajuwa alisema alisema wajane wanahitaji kusaidiwa
ili kuondokana na ombaomba na kuishi maisha ya kubabaisha.
“Namuomba Waziri awatambuwe wajane kupitia jumuia
yao kwa kukutana nao ili kuwasikiliza. Ni lazima wajane na yatima
wasaidiwe,” alisema Mwanajuma.
Naye Mwakilishi wa viti maalum vya wanawake (CCM)
Asha Bakari Makame, alilalamikiwa kuongeza kwa udhalilishaji wa
wananwake na watoto Unguja na pemba.
“Udhalilishaji na hasa ukabaji bado ni tatizo
kubwa, ni lazima serikali ifanye juhudi za kudhibiti ili kuwalinda
wanawake na watoto,” alisema Asha huku akiungwa mkono na wajumbe wengine
wa baraza hilo.
Akijibu hoja za wajumbe hao, waziri wa Ustawi wa
jamii na maendeleo ya vijana, wanawake, na watoto Zainab Omar Mohammed
aliwataka Wajumbe kuungana na serikali katika vita dhidi ya
udhalilishaji.
“Vitendo vya udahlilishaji vimekithiri sana,
lakini tunahitaji ushirikiano wa hali ya juu ili kuweza kushinda.
Serikali pekee haiwezi, na nawaomba wananchi wasione aibu kutoa taarifa
na kuja kutoa ushahidi mahakamani,” alisema Zainab.
Waziri alisema kuwa tabia ya baadhi ya wananchi
kuficha taarifa za ubakaji na kuogopa kutoa ushahidi mahakami
inazorotesha juhudi za kupambana na uhalifu huo nchini, na kushauri
elimu zaidi kwa wananchi
0 comments:
Post a Comment