Kiukweli
kitu kikubwa kinachotokea ni kwamba, Imefika kipindi sasa inabidi wasanii wa
Tanzania tuamke tuone wapi tunataka tuelekee na pia tuanze kutafakari ni wapi muziki
wetu tunataka uelekee, kwasababu tumefanya mziki huu kwa mafanikio, tumetoka
mbali kwenye sehem za hatari sana na sasa tuna advantage ya kwamba kiswahili kinaenda
kama lugha ya kimataifa tumepata mashabiki nje ya tanzania.....".
PROFESSOR JAY - Mwanamuziki Tanzania |
ndio
maana leo kwenye account yangu ya twitter nikasema, inafika kipindi sasa
tuangalie, kwasababu kila mmoja anakua anamtupia lawama mwenzake na vitu
vingine kama hivi, ni kwamba tukae kama wasanii kama watanzania tunaotaka
tuangalie mziki huu tunataka tuupeleke wapi....
Inavyoonekana
anaeuharibu huu mziki sio mtu mmoja....wasanii kama wasanii unakuta wanaandika
mashairi ambayo hayaeleweki hata kwenyejukwaa perfomance zao vingine
havisaidii kuupeleka mziki wetu mbali hata media inaonekana kucheza nyimbo
zingine ambazo kiulweli kabisa hazisaiidii chochote kwenye mziki wetu wa
Tanzania na katika harakati hizi za kuupeleka mziki wetu kwenye level,
"
"lawama
zangu pia nazipeleka kwa mashabiki, kwasababu wana nyimbo zao ambazo wanapiga
simu wanaomba, kwenye matamasha wanasapoti ya watu wengine lakini kiukweli zile
nyimbo hazisaidii chochote, mashabiki saa zingine wanaomba nyimbo ambazo hazisaidii
chochote na zinakuwa mbovu, "
"lakini
kitu ambacho kikubwa kabisa cha mwisho, ni kwamba serikali ina play part vipi
katika swala hili, ikiwa kama baba wa watanzania wote inabidi itoe
kauli,kwasababu wasanii kila siku kilio chao ni kwamba kazi zao zinaibiwa watu
wanakosa ubunifu ndio maana wanaimba vitu ambavyo viko bubble gum, na vitu
ambavyo havieleweki, serikali kama serikali ingejaribu kuangalia jinsi gani ya
kuwasaidia wasanii wa Tanzania especially katika kazi zao, kwenye vitu kama
ringtones, lakini pia katika sheria jinsi gani msanii anaweza kunufaika na kazi
zake anayoifanya, kwasababu hata sasa hivi hizi stika za TRA haziwezi kusaidia
kitu stika zitakuwepo lakini tatizo sugu tumeliacha, tatizo ni wizi wa kazi za
wasanii......." amesema Prof Jay.
0 comments:
Post a Comment