Viongozi wa dini wameaswa kuzingatia mafundisho ya dini zao kwa kuwa dini zimeletwa duniani kwa ajili ya kuwaleta pamoja wanadamu badala ya kuwa kichocheo cha kuwatenganisha na kuvuruga amani.
Rai hiyo imetolewa na waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa,SHAMSI VUAI NAHODHA wakati akifungua kongamano la siku mbili la viongozi wa dini lililoitishwa na kamati ya ulinzi na usalama na viongozi wa dini mkoa wa DSM lililoketi kujadili mustakabali wa hali ya amani katika mkoa wa DSM na nchi nzima ambapo ameongeza kuwa uislam na ukristo sio mzigo bali tutumie fursa hizo kutupa tija katika kujiletea maendeleo.
![]() |
| SAID MECK SADIKI -MKUU WA MKOA DSM |



0 comments:
Post a Comment