Baadhi ya wazazi walioitwa na mwalim mkuu wa shule hiyo wakimsikiliza mwalimu huyu juu ya watoto wao kutofika shule |
Mwalimu Mkuu wa shule ya Idugumbi Mpaze Mchaba, amesema licha ya shule hiyo kuwa na madarasa ya kutosha , madawati pamoja na walimu lakini watoto waliopo ni 270. |
SHULE ya msingi ya Idugumbi iliyopo Mbeya vijijini, inakabiliwa na uhaba wa wanafunzi kutokana na wazazi kuwatumia watoto hao kwenye shughuli za uvunaji wa zao la kahawa.
Akizungumzia
tatizo hilo, Mwalimu Mkuu wa shule ya Idugumbi Mpaze Mchaba, alisema licha ya
shule hiyo kuwa na madarasa ya kutosha , madawati pamoja na walimu lakini
watoto waliopo ni 270.
Alisema,
uhitaji wa shule ni watoto zaidi ya 400 lakini mpaka sasa ni watoto 270 ndio
wanaohudhuria masomo darasani na kati yao ni watoro wa kudumu.
Alisema,
kamati ya shule ilifanya uchunguzi na kubaini kuwa baadhi ya wazazi wamekuwa
wakiwatumikisha watoto kwenye shughuli ya kilimo kama vile kuvuna kahawa na
kupeleka viwandani.
“Baada
ya kubaini tatizo hili tulilifikisha kwenye serikali ya kijiji na kuazimia kuwa
kila mtoto atakaye toroka shule mzazi atawajibika kutoa shilingi 2000 kila siku
atakaye kosa masomo tukiamini wazazi watajirekebisha na kuwahimiza watoto
kufika shuleni hali ambayo ni tofauti,”alisema
Akizungumzia
tatizo hilo Mtendaji wa kijiji cha Idugumbi Deodath Msyaliha, amekiri kuwepo
kwa utoro wa wanafunzi pamoja na wazazi kuwatumia watoto kwenye shughuli hizo
za uzalishaji kwa kutumia kilimo cha kahawa.
Aliwataja
baadhi ya wazazi hao kuwa ni Isaya Waziri, Yohana Waziri, Julius waziri na
Msuya Waziri ambao wote kwa pamoja walikiri kwa maandishi mbele ya kamati ya
shule kuhusika na ukatishaji watoto masomo na kukubali kulipa lakini mpaka sasa
hawajatekeleza.
Aidha,
Mtendaji huyo, alisema suala hilo limefikishwa kwenye ofisi ya Mtendaji Kata na
Diwani ili watuhumiwa hao washughulikiwe kwa kuwakatisha watoto masomo darasani
kama taratibu za elimu zinavyoeleza.
Wakati
huo huo, Shule ya msingi ya Mbalizi na Mageuzi zinatarajiwa kufunguliwa hivi
karibuni baada ya kufungwa kwa zaidi ya miezi miwili kutokana na ukosefu wa
matundu ya vyoo.
Akizungumzia
hilo Mwenyekiti wa kijiji cha Mapinduzi Nelsoni Mwakyusa, alisema kijiji
kilitoa shilingi 200,000 katika kukamilisha ujenzi wa matundu 24 ya vyoo
vipya ambapo matundu ya awali yalititia kutokana na mvua za masika.
Alisema,
kutokana na tatizo hilo shule hizo hazitakuwa na likizo katika kufidia muda
ambao watoto walikaa nyumbani na kukosa masomo kwa zaidi ya miezi miwili.
Picha na E . Kamanga
0 comments:
Post a Comment