Image
Image

UMOJA WA MATAIFA KUPITIA MPANGO WA UBRAF WAENDESHA SEMINA KWA WATANGAZAJI WA RADIO ZA KIJAMII ZA AFRIKA MASHARIKI.

Bi. Stella Vuzo  - Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja  wa Mataifa (UNIC) Dar  - Es -  Salaam.

Bw. Jimmy Okello wa COMNETU akitoa tathmini ya ripoti endelevu za Radio za Kijamii nchini Uganda.

Baadhi ya wadau mbalimbali kutoka tasnia ya habari waliohudhuria semina iliyohusisha Redio za Kijamii iliyofanyika Terrat wilayani Simanjiro mkoani Manyara hivi karibuni kwa udhamini wa Umoja wa Mataifa kupitia Mpango wa UBRAF.
Washiriki wa warsha hiyo iliyowakutanisha Watangazaji wa Radio za Kijamii kutoka Kenya, Uganda, Rwanda na Tanzania wakitoa maoni yao ya namna ya kuboresha uandaaji wa vipindi vyao vya Radio za Kijamii sambamba na vikwazo wanavyokumbana navyo katika kazi zao.

Afisa Habari wa Kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Dar es Salaam Bi. Stella Vuzo akizungumzia umuhimu wa kuwa na mikakati madhubuti ya kushirikishana baina ya Waandishi wa habari na Umoja wa mataifa na pia akafafanua mpango mkakati wa Umoja wa mataifa juu ya usalama wa waandishi wa habari pindi wawapo kazini.


Picha juu na chini ni Mshauri wa Radio Jamii na Mkufunzi wa UNESCO Dar es Salaam Bi. Rose Mwalimu akiendesha majadiliano kuhusu mikakati endelevu itakayowezesha kuihusisha jamii katika program zinazohusu kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi wakati wa warsha iliyofadhiliwa na mpango wa Unified Budget Result Accountability Frame Work (UBRAF) uliochini ya Umoja wa Mataifa.











Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment