Image
Image

waziri nchimbi akutana na ujumbe wa EU kuzungumzia hali ya ulinzi na usalama

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi katika Kikao na Wawakilishi wa Nchi za Umoja wa Ulaya waliotembelea Wizarani jana.  Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil.  (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Serikali  ya Tanzania  imesema itahakikisha inaendelea kuimarisha hali ya ulinzi na usalama kwa watanzania na raia wa kigeni waliopo na wanaoendelea kutembelea hapa nchini  kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za binafsi na kimaendeleo  ili watu wote  waweze kutekeleza majukumu yao na  kuishi kwa amani na usalama hapa nchini. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi amesema hayo leo wakati akizungumza katika kikao baina yake na Ujumbe wa Wawakilishi wa nchi za Umoja wa Ulaya na mabalozi wa  nchi hizo hapa nchini kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa wizara hiyo.
Mabalozi hao ni Dk. Ad Koekkoek wa Uholanzi, Marcel Escure wa Ufaransa,  Diana Melrose wa Uingereza,  Koenaad Adam wa Belgium na Luis Cuesta wa Spain.
Kikao hicho kilichowakutanisha Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, Mkuu wa Jeshi la Polisi(IGP) Said Mwema , Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela , Kamanda wa Polisi Kanda Maalum  Dar es Salaam Suleiman Kova na Ujumbe wa Wawakilishi wa Jumuia ya Ulaya ikiongozwa na Balozi Filberto Cerani Sebregondi  kimejadili hali ya usalama katika Jiji la Dar es Salaam.
Waziri Nchimbi amesema kwa sasa serikali kupitia Jeshi la Polisi imejiwekea mikakati mbalimbali ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu katika Jiji la Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla ikiwemo kufanya kila jitihada kuhakikisha kuwa hali ya ulinzi na usalama inaimarishwa na kwamba  takwimu zinaonyesha kupungua kwa vitendo vya uhalifu.
“ Jeshi la Polisi tayari limeanzisha Dawati  Maalumu litakalowahudumia raia wa kigeni ili kuwawezesha kufungua kesi zao kwa urahisi, kuwepo kwa wepesi wa majadiliano na ziweze kushughulikiwa kwa haraka na hatimaye kupatiwa ufumbuzi”. Amefafanua Waziri Nchimbi.   
Waziri Nchimbi amesema pia katika kusimamia suala la Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao kwa sasa wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  itafanya ukaguzi wa Kampuni Binafsi ya Ulinzi  ili kuangalia na kujiridhisha kama  yanakidhi viwango vya ubora vinavyotakiwa.
Kwa upande wake Kiongozi wa Ujumbe wa Wawakilishi wa nchi za Umoja wa Ulaya hapa nchini Balozi  Filberto Cerani Sebregondi  amesema Umoja huo utaendelea kushirikiana  na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  ambapo pia ameishukuru Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa jitihada inayoendelea kuchukua  kuhakikisha ulinzi na usalama kwa wageni na raia wa nchini Tanzania.
Kwa upande wao Mabalozi waliohudhuria kikao hicho wameitaka Serikali na Watanzania kuhakikisha usalama unadumishwa ili kutoathiri taswira ya Tanzania Kimataifa na hivyo kuhatarisha uwezekaji na utalii.
 Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI,
28 Mei, 2013
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment