MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom
Kibanda anatarajia kuwasili leo akitokea nchini Afrika Kusini alipokuwa
akitibiwa tangu Machi 6, baada ya kushambuliwa na kuumizwa vibaya na watu
wasiofahamika usiku wa Machi 5.
Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na
Katibu Mkuu wa TEF, Neville Meena, Kibanda atawasili Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Nyerere leo saa 7 mchana na atazungumza na waandishi wa
habari.
Kutokana na ujio huo, Meena aliwaomba wahariri na
waandishi kufika uwanjani hapo kuanzia majira ya saa 6.00 mchana kwa ajili ya
kumpokea mwenzao huyo aliyekaa nje ya nchi kwa miezi mitatu.
“Mwenzetu kakaa Afrika Kusini kwa siku 90, hii ni fursa
nyingine adhimu ya waandishi wa habari nchini kuonyesha mshikamano na umoja
wetu kwa kwenda kumpokea,” alisema.
Kibanda ambaye pia ni Mhariri
Mtendaji wa New Habari (2006) Ltd, kuumizwa kwake kuliitikisa tasnia ya habari
nchini na kuzua mijadala mbalimbali ndani na nje ya nchi.


0 comments:
Post a Comment