TIMU ya soka ya African Lyon ya jijini Dar es Salaam imetangaza
hasara ya sh. milioni 180.3 kutokana na ushiriki wake katika msimu uliopita wa
Ligi Kuu Tanzania Bara.Lyon ni miongoni mwa timu tatu zilizoshuka daraja kutoka
katuika ligi hiyo kubwa ya soka nchini, nyingine ni Toto African na Polisi
Moro.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es
Salaam, Meneja wa Fedha wa Lyon, Ibrahim Salim, alisema timu yao imetumia zaidi
ya sh. 388,614,500 kwa ajili ya maandalizi hadi michezo yake.
Salim
alisema katika makusanya na matumizi yao, walilazimika kutumia kiasi cha sh.
milioni 268.09 katika mzunguko wa kwanza, kabla ya kutumia sh. 123.6.“Katika
matumizi yote haya, fedha ambayo tumeiingiza kama klabu kupitia viingilio na
vyanzo vingine ni sh. milioni 207.6, na hapo ndipo unapopata tofauti ya sh.
milioni 180.3, ambayo ni hasara,” alisema Salim.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Lyon, Rahim Kangezi,
alisema soka ya Tanzania inaendeshwa kwa hasara huku wenye dhamana ya kusaidia
wakiwa hawatendi haki kwa baadhi ya vipengele.
Kangezi alisema timu yake imeingia katika hasara ya sh. milioni
180.3 kutokana na uendeshaji, lakini bado wameshuka daraja, huku akisisitiza
kuwa hakuna anayeshutumiwa kwa kushuka kwa timu hiyo.
“Unaweza kuona changamoto ambayo tunakumbana nayo katika
uendeshaji wa taasisi kamam a hizi, tunapopiga kelele kwa wadhamini
kutuwahishia fedha tunamaanisha.
“Angalieni mfano mdogo kwa fedha za wadhamini (Vodacom), ambazo
awamu ya mwisho zimetufikia Mei mwaka huu, tukiwa tumebakiza mechi moja ya Ligi
Kuu, sasa zingetusaidia katika nini? Alihoji mmiliki huyo.
Akizungumzia kuhusu uendeshwaji wa Ligi Kuu na changamoto
walizokutana nazo, Kangezi alisema bado hakujakuwa na usimamizi mzuri katika
kuhakikisha kuwa ligi hiyo inakuwa bora.
Katika hatua nyingine, Kangezi alisema timu yake inajivunia
mafanikio waliyochangia kusogeza maendeleo ya soka nchini kutokana na kutoa
nafasi kwa Mrisho Ngassa kwenda kujaribu soka ya kulipwa na kucheza katika
kikosi cha Seattke Soundowns dhidi ya Manchester United.
“Tulifanikiwa pia kuileta timu kubwa ya Ligi Kuu ya Brazil
(Atletico Parenese) kwa ziara ya kimichezo nchini, tulitoa wachezaji watano kwa
ajili ya kujaribu soka ya kulipwa sambamba na kufanya semina mbili juu ya
uongozi wa michezo,” aliongeza.


0 comments:
Post a Comment