Timu mbili pinzani katika soka la nchini Misri Al
Ahlyna Zamalek zinatarajia kuanza kampeni yao za kuwania taji la vilabu
barani Afrika baada ya kukutana na kukubaliana juu ya eneo na uwanja
utakaotumika katika mchezo wao utakaochezwa.
Vilabu vyote hivyo maskani yao ni katika jiji la Cairo,
zitakuwa zikikutana katika mchezo wa ufunguzi wa kundi wa A huko katika uwanja
wa El Gouna maeneo ya Red Sea.
Makubaliano juu ya uwanja utakao tumika yamefikiwa kutokana
na sababu za kiusalama kutokana na nchini hiyo kukumbwa na hali isitulia
kisiasa ambapo mchezo huo uliahirishwa wiki iliyopiya kutokana na sababu za
kibiashara"marketing reasons".
Pande zote mbili zimewaita nyota wao muhimu katika sehemu ya
kiungo akiwemo Mohamed Aboutrika kwa upande wa Ahly and Mahmoud Abdel Razak kwa
upande wa Zamalek.
Aboutrika, anatazamwa kama ni mmoja wa wachezaji wakubwa
kabisa kuwahi kuchomza katika soka la ukanda wa Afrika Magharibi akiwa
ameshakamilisha kipindi chake cha mkopo katika klabu ya Baniyas ya Falme za
kiarabu.
Kiungo mwenye kipaji "volatile" Abdel Razak,
akijulikana zaidi kama 'Shikabala', pia amekuwepo kwa mkopo huko falme za
kiarabu katika klabu ya Al-Wasl miezi nane iliyopita.
Wote hawa ni wachezeshaji ambao wamekuwa wakifanya kazi ya
kuendesha sehemu ya kiungo katika vilabu vyenye mafanikio makubwa barani Afrika
katika michuano mikubwa ya Confederation na champions huku Ahly wakishinda
mataji ya vilabu Afrika mara 16 nao Zamalek mara tisa.
Hata hivyo vikosi vyote vitawakosa wapiga mabao wao hodari
Emad Moteab kwa upande wa Ahly mwenye majeraha na kwa upande wa Zamalek wao
watamkosa Abdoulaye Cisse ambaye ameihama Zamalek.
Kutokana na sababu za kiusala kuwa ndogo kufuatia kuangushwa
kwa utawala wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Mohamed Morsi mchezo huo sasa
utapigwa katika uwanje wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 12,000 na usiokuwa na
usiokuwa na taa za kutosha mchezo huo sasa utalazimika kuchezwa mchana kweupe.
Inaarifiwa kuwa hali hiyo itawasumbua sana wachezaji ambao wengi
wao wako katika funga ya mwezi wa Ramadhani.
Licha ya kwamba wachezaji wa timu hizo wameruhusiwa kula na
kunywa katika siku ya mchezo lakini wengi wanaamini kuwa bado
haitawajenga vizuri katika imani kutokana na imani ya dini zao
0 comments:
Post a Comment