Hali ya uchafu katika jiji la Dar es Salaam. |
Makamu wa Rais Dr.Mohamed Gharib
Bilal leo ameanza ziara ya kutembelea maeneo mbali mbali ya jiji la Dar es
Salaam kuangalia hali ya usafi na mazingira ambapo katika maeneo kadhaa
alikumbana na malalamiko kutoka kwa wananchi kutokana na hali mbaya ya uchafu
huku viongozi wa maeneo husika wakishindwa kuwajibika.
Dr.bilal akiwa amefuatana na waziri
mwenye dhamana ya mazingira, mkuu wa mkoa wa dar es salaam pamoja na viongozi
wa wilaya alitembelea kituo cha mabasi yaendayo mikoani kilichopo mbagala
ambapo alijionea hali ya usafi pamoja na kuzungumza na vijana wanaoshiriki katika
vikundi vya ulinzi shiriki.
Aidha katika soko la buguruni makamu
wa rais alikumbana na malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara waliodai kuwa soko
hilo limekithiri kwa uchafu ,wengine wakidai kuwa soko hilo ni chakavu ,ambapo
katika dampo la Pugu wananchi wamesema wanalazimika kula chakula ndani ya
chandarua kutokana kukithiri kwa Inzi eneo hilo.
Akizungumzia hali ya usafi Makamu wa
rais amewataka viongozi wa manispaa na mkoa kuhakikisha jiji la dsm linakuwa
safi kwa kuhakikisha wanawashirikisha wananchi katika utekelezaji .
Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais mazingira Dr.Teresia huviza amesema viongozi wa mkoa na manispaa za jiji la dsm wameshindwa kusimamia hali ya usafi hivyo kusababisha maeneo mengi hasa ya biashara ,kando za barabara kukithiri uchafu hali inayoweza kuhatarisha afya za wakazi wa jiji la dsm.
Dr.Teresia huviza - Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais Mazingira |
0 comments:
Post a Comment