Barcelona imemtangaza raia wa Argentina
Gerardo Martino kama kocha wake mpya baada ya kukubali kuingia mkataba wa miaka
miwili.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 50
ambaye ni bosi wa zamani wa timu ya taifa ya Paraguayanachukua nafasi ya Tito
Vilanova ambaye aliachia ngazi nafasi hiyo ili kuweza kuendelea na matibabu ya
Kansa.
Martino ndiye kocha wa hivi karibuni
wa Newell's Old Boys, ambao walitwaa taji la nchini Argentina la Clausura msimu
uliopita
Gerardo Martino factfile
- 1962: Alizaliwa Novemba 20 huko Rosario, Argentina
- Akiwa mchezaji: Anashikilia rekodi ya kuichezea michezo mingi klabu ya Newell's Old Boys akicheza jumla ya michezo 505 vilevile akiitumikia timu ya taifa ya Argentina pamoja na kucheza soka nchini Hispania, Ecuador na Chile kabla ya kustaafu kucheza soka mwaka 1996.
- Kazi ya umeneja: Alianza na vilabu vidogo nchini Argentina ya Brown de Arrecifes, Platense na Instituto kabla ya kutwaa taji la ligi ya Paraguay akiwa na Libertad na Cerro Porteno.
- Paraguay: Alichukua nafasi ya kuifundisha timu ya taifa ya Argentina mwaka 2006 na miaka minne baadaye aliipeleka mpaka katika hatua ya robo fainali ya kombe la dunia ambako walifungwa na waliokuwa mabingwa wa taji hilo timu ya taifa ya Hispania. Aliondoka katika timu hiyo baada ya kushika nafasi ya pili nyuma ya Uruguay waliokuwa mabingwa mwaka 2011 michuano ya Copa America.
- Newell's Old Boys: Alirejea katika kazi ya kufundisha katika timu yake ya zamani kufundisha mwaka 2012 na kuingoza na kushinda taji la ligi ya Argentina Clausura.
- Barcelona: Anakuwa meneja wa nne raia wa Argentina kuingoza Katalunya baada ya Tito Vilanova
Anakuwa meneja wa wanne baada ya
Helenio Herrera, Roque Olsen na Cesar Luis Menotti.
Kazi ya kuifundisha Barcelona
kwake Martino inakuwa ni kazi ya kwanza kufundisha soka nje ya Amerika ya
kusini tangu alipooondoka nchini humo baada ya kuitumikia klaby ya Tenerife mwaka 1991.
Kulikuwepo na makocha kadhaa
waliokuwa wakihusishwa na kazi hiyo akiwemo bosi wa zamani wa Barcelona B Luis
Enrique, bosi wa Tottenham Andre Villas-Boas, bosi wa Swansea Michael Laudrup na Guus Hiddink
ambaye aliachana na kazi ya kuifundisha Anzhi Makhachkala jumatatu.
Nahodha wa Barcelona Carles Puyol anasema aina ya
utawala wa Martino utaoana na philosophy ya Nou Camp.
0 comments:
Post a Comment