SHIRIKA
la kutetea haki za kibinadamu la Human Rights Watch limesema kuwa kundi la
wapiganaji la M23 Mashariki mwa Jamhuri ya Demokrsia ya Congo limewaua zaidi ya
watu arobaini na kuwabaka zaidi ya wanawake na wasichana sitini tangu Machi
mwaka huu.
Baada
ya kuwahoji zaidi ya watu mia moja eneo hilo, shirika hilo lilisema kuwa waasi
hao wanawasajili kwa nguvu vijana huko DRC na wengine kutoka nchi jirani ya
Rwanda.
Kundi
hilo limeongeza kuwa Jeshi la Rwanda bado linawasadia moja kwa moja waasi hao
licha ya serikali ya Kigali kupinga hilo mara kwa mara. (HM)
Wakati
huohuo, jeshi la DRC hapo jana lilishambulia ngome za waasi hao karibu na mji
wa Goma Mashariki mwa DRC.
Haya
yalikuwa mashambulizi ya kwanza tangu vita kati ya pande hizo mbili kuanza
Jumatatu asubuhi na kusitishwa siku hiyo mchana.
Kundi
hilo limesema liko umbali wa kilomita nne kutoka mji wa Goma, ingawa limesema
lengo lake ni kulazimisha serikali kufanya mazungumzo nao wala sio kuteka mji
wa Goma.
M23
liliuteka mji wa Goma, kwa siku kumi mwezi Novemba kabla ya kuondoka mjini humo
kufuatia shinikizo za jamii ya kimataifa kufanya mazungumzo na serikali ya rais
Joseph Kabila.
Mazungumzo
na serikali yalianza mjini Kampala mwezi Disemba ingawa baada ya miezi miwili
jeshi likaanza tena mapigano na waasi hao mwezi Julai tarehe 14.
Kulingana
na Umoja wa Mataifa mapigano hayo yamesababisha takriban watu 4,200 kutoroka
makwao.
0 comments:
Post a Comment