Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mtwara
Linus Simzumwa amekanusha taarifa za kuvamiwa na kupigwa mawe na watu
wasiojulikana gari lililokuwa limebeba mabomba ya mradi wa ujenzi wa
kusafirishia gesi asilia kutoka mtwara kwenda Dar .
Linus Simzumwa Kamanda wa polisi Mtwara. |
Likiwa limebeba mabomba sita kuyapeleka
kituo cha Kilanjelanje mkoani Mtwara ikiwa ni maandalizi ya ujenzi wa mradi huo
wa bomba, kioo cha mbele cha roli la kampuni kutoka China ya CPDC inayojenga
bomba hilo kilivunjwa kwa jiwe.
Akitolea ufafanuzi tukio hilo, Kamanda
Simzumwa amesema kuvunjika kioo cha mbele cha lori hilo kulitokana na mwendo
kasi wa kupishana kwa magari na kwamba jeshi hilo linaendelea na upelelezi.
Kwa upande wake dereva wa roli hilo Said
Mohammed pamoja na kuthibitisha kuvunjwa kwa kioo cha gari hilo amesema
hafahamu chanzo cha kutokea kwa jiwe hilo.
Shughuli za ujenzi wa bomba la gesi
zimeanza rasmi kwa kampuni ya china kueneza mabomba hayo kwenya kambi zilizotengwa.
Aidha amemwomba Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said
Mwambungu kuligeuza soko hilo kuwa la kimataifa zaidi bila kuchagua
mfanyabiashara mdogo au mkubwa.
0 comments:
Post a Comment