Huyu ni Amani (39) - Baba aliye mlawiti mwanae wa kumzaa.
Mahakama ya wilaya ya Mbeya imemhukumu kwenda jela miaka
30 mkazi wa Isanga Mkoani hapa baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumlawiti na
kumzalisha binti yake wa kumzaa akiwa na miaka 15( jina linahifadhiwa).
Mwendesha mashitaka wa serikali Archiles Mulisa
aliiambia mahakamani hiyo Mbele ya Hakimu Gilbert Ndeuruo kuwa Mshtakiwa
huyo ni Yusufu Amani (39) anayedaiwa kumbaka mwanaye wa kumzaa kisha kumzalisha
baada ya kutengana na mkewe.
Alisema kosa hilo ni kinyume cha sheria kifungu cha 154 (1)a na
155 sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, pamoja na kifungu cha
158(a) cha makosa ya kuzini.
Akisoma Hukumu hiyo Hakimu Ndeuruo alidai kuwa Mtuhumiwa alianza
kujihusisha kimapenzi na mwanaye Mwaka 2008 baada ya kutengana na mkewe ambapo
Mtuhumiwa aliachiwa watoto wote.
Aliongeza kuwa wakati huo binti huyo alikuwa na umri wa
miaka 12 na alikuwa akisoma shule ya msingi darasa la Tano jambo ambalo
wamedumu nalo kwa Miaka mine hadi ilipogundulika kuwa binti alikuwa mjamzito
Mei, 2012.
Alisema mbinu aliyokuwa akiitumia ni kumtishia binti
asitoe taarifa kwa mtu yoyote na kwamba baada ya kugundulika kuwa na ujauzito
alimwambia amsingizie kijana yoyote mtaani kwao.
Hakimu Ndeuruo alisema Mahakama ilimtia hatiani
Mtuhumiwa kutokana na ushahidi wa Mhanga wa tukio hilo ambaye ni binti pamoja
na ushahidi wa kitaalamu kutoka kwa Mkemia mkuu wa Serikali.
Alisema ushahidi wa Mkemia Mkuu wa Serikali baada ya
kupima Vinasaba kutoka Mtuhumiwa, Mhanga na Mtoto aliyezaliwa ulidai kuwa
Mshtakiwa ndiye baba halali wa Mtoto kutokana na Maeneo 15 ya vipimo vya
Vinasaba kati ya Baba na Mtoto aliyezaliwa kufungana kwa asilimia 99.9.
Aidha kabla ya kutoa hukumu Hakimu alimpa nafasi
mtuhumiwa kujitetea ili apunguziwe adhabu au asiweze kuhukumiwa kabisa lakini
hali ikawa tofauti baada ya Mtuhumiwa kujibu kuwa hana la kujitetea vyovyote
itakavyokuwa anachotaka ni nakala ya hukumu.
Kutokana na kushindwa kujitetea Hakimu Ndeuruo
alimhukumu kwenda jela miaka 30 na kwamba ana haki ya kukata rufaa katika
Mahakama kuu endapo hakuridhika na hukumu hiyo.
Awali katika ushahidi wake Mahakamani hapo Mtuhumiwa
huyo alidai kuwa hakutenda kosa hilo bali alitengenezewa na Mkewe ambaye aliapa
kumkomesha baada ya kukosana na kumpata mume mwingine jambo ambalo lilipingwa
vikali na hakimu na kudai kuwa “ mfa maji haachi kutapatapa”
Na Mbeya yetu
0 comments:
Post a Comment