Freeman Mbowe |
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe jana alihojiwa tena na Jeshi la Polisi, lakini akaendelea na msimamo wake kwa kugoma kuwasilisha ushahidi wake kuhusu mlipuko wa bomu uliotokea mkoani Arusha Juni 14, mwaka huu.
Mbowe
alifika Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam kuitikia wito wa jeshi hilo kumtaka
awasilishe ushahidi wake aliosema kuwa anao, lakini aligoma akisema atautoa
pale tume ya kijaji itakapoundwa na Rais Jakaya Kikwete kama alivyoomba.
Kiongozi
huyo wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alitaka kuundwa kwa tume huru ili kuchunguza
mlipuko huo uliotokea alipokuwa akihitimisha hotuba yake katika mkutano wa
mwisho wa kampeni za udiwani kwenye Viwanja vya Soweto, Arusha.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Chadema, John Mnyika alisema jana kuwa Mbowe alikwenda polisi
baada ya kuandikiwa barua ya kumtaka afike kuwasilisha ushahidi. Alifika lakini
aligoma kutoa ushahidi huo.
“Alikwenda
tu kuitikia wito wa polisi uliomtaka awasilishe ushahidi, lakini amegoma
kufanya hivyo na amewaeleza polisi kuwa hatafanya hivyo hadi Rais atakapounda
tume ya kijaji kama alivyomwandikia barua,” alisema na kuongeza: “Anachosubiri
sasa ni majibu ya Rais kuhusu barua yake.”
Mnyika
alisema baada ya maelezo hayo, Mbowe alitakiwa kuyaweka kimaandishi kupitia kwa
wakili wake Peter Kibatala na kuyawasilisha polisi ifikapo kesho.
Akizungumzia
suala hilo, Wakili Kibatala alisema: “Mbowe ameachiwa baada ya majadiliano ya
kisheria kati yangu na Kamanda Advocate Nyombi.
Tumekubaliana kujibu kwa maandishi wito wa polisi walioutoa kwake wakimtaka awasilishe ushahidi wa kuhusika kwa polisi katika mlipuko wa bomu Arusha na kisha kuyafanyia kazi hayo kisha kutuarifu.”
Tumekubaliana kujibu kwa maandishi wito wa polisi walioutoa kwake wakimtaka awasilishe ushahidi wa kuhusika kwa polisi katika mlipuko wa bomu Arusha na kisha kuyafanyia kazi hayo kisha kutuarifu.”
Msemaji
wa Polisi SSP, Advera Senso alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema anafuatilia
kujua kama kweli Mbowe alihojiwa na kama kutakuwa na habari ya kuwajulisha
wananchi ataitoa baadaye.
Wiki
iliyopita jeshi hilo lilimhoji Mbowe kwa madai kuwa kauli zake alizozitoa baada
ya mkutano wa Kamati Kuu ya chama hicho ni za uchochezi.
Mbowe
ambaye pia ni Mbunge wa Hai alihojiwa kutokana na madai aliyosema kwamba polisi
ndiyo waliohusika na ulipuaji wa bomu Arusha, pia polisi kusaidia CCM kwenye
uchaguzi na kumtuhumu Rais Jakaya Kikwete kuhusika na mauaji ya Arusha kutokana
na kukaa kwake kimya.
MWANANCHI.
0 comments:
Post a Comment