Image
Image

NESTA AMBAYE NI MLINZI WAZAMANI WA KIMATAIFA WA ITALIA ASEMA KUWA LIGI KUU YA SOKA NCHINI HUMO YASHINDWA KUFUA DAFU.


Mlinzi wa kati wa zamani wa kimataifa wa Italia Alessandro Nesta amesema ligi kuu ya soka nchini humo Serie A imeshindwa kufua dafu kwa ubora mbele ya ligi nyingine za barani Ulaya ikiwemo ligi ya Hispania, Ujerumani na England.

Nesta ambaye kwasasa ana umri wa miaka 37 kwasasa anachezea soka katika klabu ya Montreal Impact inayoshiriki ligi kuu ya Marekani MLS.

Akiwa bado nchini Italia Nesta aliwahi kushinda taji la Italia maarufu kama Scudetto mara tatu akiwa na vilabu vya Lazio na AC Milan.

Nesta ametoa sababu ya kushindwa kwa ligi hiyo ya Italia na ligi nyingine ni kwamba kumetokana na kukosekana kwa fedha.

Akinukuliwa amesema
"Hakuna pesa kwasasa inchini Italia na hivyo wachezaji wazuri wamekuwa akikimbilia kucheza soka katika ligi za Hispania , England na Ujerumani. Ligi ina poromoka"

Nesta, ambaye pia alishinda taji la kombe la dunia mwaka 2006, ameshangazwa na klabu ya Juventus kufanikiwa kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Carlos Tevez kwa ada iliyotajwa kuwa ni pauni milioni £12.

Amesema klabu hiyo imefanya usajili bora kwa kudaka saini ya Tevez, na kwamba hakuwahi kufikiria mchezaji kama Tevez kuelekea katika ligi ya Italia Serie A kwasasa. Amesema Juventus imefanya kazi kubwa.

Nesta anataka kuelekea katika kazi ya ukocha itakapo fikiwa wakati wake wa kustaafu kucheza mwishoni mwa msimu ujao wa ligi kuu ya Marekani.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment