Mlinzi wa
kati wa zamani wa kimataifa wa Italia Alessandro Nesta amesema ligi kuu ya soka
nchini humo Serie A imeshindwa kufua dafu kwa ubora mbele ya ligi nyingine za
barani Ulaya ikiwemo ligi ya Hispania, Ujerumani na England.
Nesta
ambaye kwasasa ana umri wa miaka 37 kwasasa anachezea soka katika klabu ya
Montreal Impact inayoshiriki ligi kuu ya Marekani MLS.
Akiwa
bado nchini Italia Nesta aliwahi kushinda taji la Italia maarufu kama Scudetto
mara tatu akiwa na vilabu vya Lazio na AC Milan.
Nesta
ametoa sababu ya kushindwa kwa ligi hiyo ya Italia na ligi nyingine ni kwamba
kumetokana na kukosekana kwa fedha.
Akinukuliwa
amesema
"Hakuna
pesa kwasasa inchini Italia na hivyo wachezaji wazuri wamekuwa akikimbilia kucheza
soka katika ligi za Hispania , England na Ujerumani. Ligi ina poromoka"
Nesta,
ambaye pia alishinda taji la kombe la dunia mwaka 2006, ameshangazwa na klabu
ya Juventus kufanikiwa kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Carlos Tevez
kwa ada iliyotajwa kuwa ni pauni milioni £12.
Amesema
klabu hiyo imefanya usajili bora kwa kudaka saini ya Tevez, na kwamba hakuwahi
kufikiria mchezaji kama Tevez kuelekea katika ligi ya Italia Serie A kwasasa.
Amesema Juventus imefanya kazi kubwa.
Nesta anataka kuelekea katika kazi ya ukocha itakapo fikiwa wakati wake
wa kustaafu kucheza mwishoni mwa msimu ujao wa ligi kuu ya Marekani.


0 comments:
Post a Comment