Amiri Jeshi Mkuu, Rais Dk, Jakaya Kikwete, ametoa wiki mbili kwa watu wanaojihusisha
na vitendo vya ujambazi, wakiwamo wanaomiliki silaha kinyume cha sheria na
wahamiaji haramu kujisalimisha na silaha zao.
Alisema
kwa kuwa amechoshwa na matukio yao, baada ya hapo kwa wale watakaoshindwa
kutekeleza amri hiyo, msako mkali utakaofanyika ukiyahusisha majeshi yote utawanasa.
Dk.
Kikwete alitoa tamko hilo jana wakati akihutubia wananchi wa Wilaya ya
Biharamulo, baada ya kuweka jiwe la msingi katikabarabara ya Kagoma- Lusahunga
inayojengwa na Serikali kwa asilimia 100.
“Nasema
mchana kweupe, macho makavu nimechoshwa na kukasirishwa na vitendo
vinavyofanywa na baadhi ya watu vya kuteka magari katikati ya pori la
Kasindaga, sasa nawataka wale wote walio miongoni mwa makundi niliyotaja
wachukue maamuzi haraka...Watanzania hatuwezi kukubali wasafiri bila
amani,” alisema Kikwete.
“Sina
mzaha kwa hili atakayekaidi kufuata ushauri huo, baada ya wiki mbili
utaanzishwa msako mkali, tutawasaka msituni, majumbani hadi wanapoficha silaha
zao na risasi. Msako huo utahusisha majeshi yote likiwemo jeshi la polisi,
jeshi la wananchi na usalama wa Taifa na vyombo vingine vya ulinzi na usalama
tutawasaka kotekote, hakuna mahali pa kukimbilia...,” alisema.
Alisema
hali ya ujambazi imekithiri katika mikoa ya Geita, Kagera na Kigoma. Alisema
lengo la msako huo ni kukomesha vitendo hivyo ambayo vimekuwa kero kubwa kwa
wananchi wanaotumia barabara hiyo.
“Ole wao
watakaowafyatulia risasi askari wangu, wakamatwe mateka na jeshi kwa lugha ya
kijeshi mtanielewa," alisisitiza.
Aidha,
aliwatahadharisha Watanzania wanowahifadhi na kushi
rikiana
na majambazi hao waache mara moja na kutafuta kazi nyingine ya kufanya kabla
hawajakumbwa na dhahma hiyo.
Wakati
huo huo, Rais Kikwete aliweka jiwe la msingi katika barabara ya Kagoma
Lusahunga yenye urefu wa kilomita 154 iliyojengwa kwa ufadhili wa Serikali kwa
silimia 100.
Alisema
kuwa lengo la kujenga barabara kwa kiwango cha lami ni kuhakikisha Tanzania
inafunguliwa kiuchumi.
Aliwashauri
wakandarasi wa Tanzania kuiga mfano wa kampuni iliyojenga barabara ya
mfano kutoka China (Chico) kwa kazi nzuri yenye viwango.
Aliiomba
kampuni hiyo kuwa wavumilivu wakati Serikali ikiendelea kushughulikia madai yao
ya Sh. bilioni 40 zilizobaki Serikali.
Rais
alitoa kauli hiyo baada ya Waziri wa Ujenzi, John Magufuli kumweleza kuwa
hajawahi kumsifia mkandarasi yeyote lakini hao wamefanya kazi nzuri, na
kuonyesha moyo huku wakitarajia kukamilisha mradi huo kwa wakati kwa muda wa
miezi 36 kama ilivyopangwa.
Kwa
upandewa Mtendaji mkuu wa wakala wa barabara Tanzania (Tanroad), Alon
Mugale, alisema mradi huo ulianza mwaka 1995 ikiwa ni upembuzi yakinifu na kwa
sasa imefikia asilimia 96 ya ujenzi.
Alisema
kilomita 153.5 zimekamilika bado meta 500 zitakazokamilika mwishoni mwa mwezi
Agosti, mwaka huu na kugharimu Sh. bilioni 191.4.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment