Polisi waliingia katika mkusanyiko wa usiku wa wafuasi wa
Morsi saa chache baada ya waziri wa mambo ya ndani kusema wafausi wa Morsi na
chama chao cha Musl
im Brotherhood waliokusanyika kwenye viunga vya msikitini wa
Rabba Al Adawiya lazima waondoke.
Muslim Brotherhood wamelilaumu jeshi kwa kuwapiga risasi na
kuwauwa wafuasi wao.
Daktari katika hospitali ya muda amesema watu wawili
walifikishwa wakiwa kichwa na viwili wili vyao vimetenganishwa huku wengine
wakiwa na matundu ya risasi vichwani na kifuani.
Hospitali hiyo imekuwa katika hali ngumu ya kumudu miili ya
marehemu na majeruhi wanaofikishwa hospitalini hapo.
Mwandishi wa BBC anasema ni mapigano mabaya zaidi tangu
jeshi limuondoe rais Morsi madarakani.
Wakati huo huo, Uingereza imekemea matumizi ya nguvu
yanayopoteza maisha ya watu nchini Misri.
Waziri wa masuala ya kigeni William Hague amewataka wenye
mamlaka kumaliza mapigano na vurugu hizo.
Amesema wale waliohusika na mauaji hayo ni lazima wawajibike
na haki ya wanaoandamana kwa amani ni wajibu ilindwe.
Bwana Hague pia amelitaka jeshi kuwachilia huru viongozi wa Muslim
Brotherhood waliowekwa kizuizini akiwemo rais Mohamed Morsi. BBC.
0 comments:
Post a Comment