Drogba akimpeleka sokoni kipa wa Arsenal, Wojciech Szczesny
Kama kawaida rafiki wa nyavu: Drogba
alifumania nyavu mara mbili na kutwaa taji la kombe la Emirates
Furaha tupu: Walcott akishagilia na wenzake
Daah!
hata kakombe haka kananishinda: Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger
akitazama vijana wake wakiburuzwa.
Didier Drogba “Tembo” amekumbukia enzi hizo akiwa ndani ya jezi ya
Chelsea akiifunga Arsenal baada ya nyota huyo mwenye miaka 35 kwa sasa
kuifungia klabu yake ya Galatasaray ya Uturuki mabao mawili kwenye
ushindi wa mabao 2-1 katika mechi ya fainali ya kombe la Emirates na
kutwaa taji hilo.
Kiukweli mechi hiyo ilikuwa ya kirafiki zaidi na haikuwa na thamani
yoyote katika msimu, lakini Drogba ameonesha tena umwamba wake wa kuwafunga
vijaba wa Arsene Wenger kwani alifanya kazi hiyo mara nyingi zaidi wakati ule
akicheza ligi kuu soka nchini England.
Kocha wa Arsenal, mzee Wenger alionekana akilaumu sana kama mechi hiyo
ni muhimu mno baada ya kumfuata na kumfokea kamisaa wa mechi hiyo Andre
Marriner kutokana na kitendo cha mwamuzi wa kati wa mechi hiyo, Jon Moss
kutoa mkwaju wa penati kufuatia beki wake
Ignasi Miquel kumfanyia madhambi mshambulaiji huyo raia wa Ivoru
Coast.
Kikosi cha Arsenal: Szczesny, Jenkinson, Sagna, Mertesacker,
Gibbs (Miquel 69), Arteta, Ramsey, Oxlade-Chamberlain, Cazorla (Zelalem 61),
Walcott, Sanogo (Giroud 61)
Goli: Walcott 38
Wachezaji wa akiba: Martinez, Koscielny, Podolski, Akpom
Kikosi cha Galatasaray; Muslera; Semih, Riera, Chedjou, Eboue,
Melo (Sarioglu 66), Engin Baytar (Gulselam 32),Altintop (Colak, 45),
Amrabat, Elmander (Drogba 45)Umut Bulut (Sneijder 45)
Wachezaji wa akiba: Nounkeu, Balta, Kazim-Richards, Kilic, Kurtrlus,
Iscan
Mabao: Drogba pen 79, 88
Mwamuzi:
Jon Moss
0 comments:
Post a Comment