Eliah Ruzika Mpiga Picha wa channel 10 akiwa amefungwa pingu na polisi.
Ikiwa zimepita Siku siku mbili sasa baada ya askari polisi
kumshambulia na kumpiga mpiga picha wa kituo cha Television cha Channel ten,
kumchania nguo zake, kumnyang'anya kamera na hatimaye kumfunga pingu
,wanaharakti mbalimbali wamelaani kitendo hicho na kusema kwamba ni kinyume cha
sheria na haki za binadamu.
Katika mahojiana maalum na TAMBARARE HALISI iliyotaka kufahamu ninamnagani wanaharakati hao na watu mbali mbali walivyo lipokea tukio hilo lililompata mwandishi huyo akiwa kazini, wanaharakati
hao,wamelaani kitendo hicho na kukiita kuwa ni cha matumizi yasiyostahiki ya nguvu
nyingi kupita kiasi kwa mtu ambaye alikuwa akitekeleza wajibu wake wa kupata
habari ili kuifahamisha jamii ambayo kimsingi ina haki ya kuhabarishwa.
Wanaharakati hao kutoka Jukwaa la
katiba Tanzania na mtandao wa mashirika yanayotoa huduma za kisheria TANLAP, nao walizungumzia namnawalivyo fadhaishwana kitendo hicho ambacho wamekiita si cha kiungwana ambapo hapa DUES KIBAMBA - M/kiti Jukwaa la Katiba ANASEMA.
"Huyu ni mwanahabari alikuwa nakusanya taarifa kwa ajili ya kuwapelekea watanzania kwa hiyo mimi
nimetoa wito na narudia tena leo kwambaa matatizo ya kisiasakama kuna asasi
inagombana na asasi nyingine au kundi moja lina ugomvi Fulani huo sio mgogoro
wa kiusalama” Alisema.
"Kitendo alicho fanyiwa ni kinyume cha
katiba yetu ya mwaka 77 ambayo inatumika hadi sasa inakataza kuteswakwa mtu
haswa awapo kazini na kazi yake anayoifanya” alisema.
GEORGE MOLLEL - TANLAP ANASEMA.
"Maamuzi ya nguvu mikonono bila kujua
kwamba nini tatizo,, kama alikuwa na kosa basi angetakiwa kufikishwakwenye
vyombo husika nasheria ikafuata mkondo wake lakini sio kumpiga mtu au akiwa
kazini” alisema.
Mpiga picha huyo, Eliah Ruzika, alikumbwa na mkasa huo kwenye ofisi za Mamlaka ya reli ya Tanzania na Zambia TAZARA ofisi ya Dar es Salaam kwa ajili ya kupiga picha mkutano wa wafanyakazi ulioundaliwa na wafanyakazi hao kwa lengo la kuelezea mgogoro uliopo kati yao na utawala wa shirika hilo.
Wakiwa kwenye chumba cha mkutano,
askari hao waliingia na kuwaamuru wafanyakazi hao waondoke kwa kuwa mkutano wao
haukuwa na na hapo ndipo yalipozuka mabishano kati ya wafanyakazi na polisi
kuhusu uhalali wa mkutano huo.
0 comments:
Post a Comment