Mkurugenzi wa michezo wa
klabu ya Barcelona sporting Andoni Zubizarreta amesema kwamba Manchester United
imeachana na mpango wa kumsaini Cesc Fabregas.
United walituma ofa mbili
zilizokataliwa na Barcelona kwa ajili ya kumsaini kiungo huyo mwenye miaka 26
na Barca wamekuwa wakirudia mara kwa mara kwamba hazuwi.
Huku kukiwa na tetesi kwamba
United wanajiandaa kutuma ofa ya tatu, Zubizarreta ameliambia gazeti la Marca
kwamba United wameachana na mpango wa kumsajili Cesc.
"Manchester United
wameonyesha kuvutiwa na mchezaji, lakini pia wameshaelewa kwamba hatutaki
kumuuza.
"Wameshaondoa suala hilo
mezani. Hatumuuzi Cesc Fabregas."
0 comments:
Post a Comment