Hawa ni
badhi yawaumini wa dini ya Kiislamu wa dhehebu la Answar suni wakiwa katika swala
ya pamoja katika kiwanja cha Ngoma Jijini Mbeya Leo.
Waumini
wa dini kiislamu madhehebu ya Answar
Sunna mkoani Mbeya wameswali swala ya Idd leo katika Viwanja vya
Kiwanja Ngoma na kuwataka Mashekhe kutotumia lugha za
uchochezi zinazojenga chuki baina ya Waislamu.
Akizungumza
na umati wa waislamu waliojumuika katika ibada hiyo ya kukamilisha kwa
mfungo wa mtukufu wa Ramadhani, imamu aliyeswalisha swala hiyo Shekhe
Ibrahimu Bombo alisema kuwa baadhi ya Mashekhe wakubwa wamekuwa wakitumia vyombo vya
habari kujenga chuki kwa waislamu.
Alisema,
swala la ibada ni wajibu kwa waislamu wote na kwamba yapo mambo ambayo
waislamu wanatofautiana katika kufanya ibada maalumu ambayo hutokana na
uelewa na kwamba jambo hilo halipaswi kuleta mgongano baina ya waislamu.
‘’Wapo mashekhe
wa taasisi fulani hujitokeza katika vyombo vya habari na kuleta kejeli
dhidi ya wengine kuhusu uelewa wa mambo, hakuna mamlaka iliyo juu ya
sheria inayopaswa kuwakejeli ama kuwatukana wengine, jambo hili lisipoangaliwa
linaweza kuleta chuki,’’alisema Shekhe Bombo.
Alisema uislamu
unajengwa kwa umoja na mshikamano na kama yapo mambo ambayo waislamu
wanapishana yanapaswa kujadiliwa kulingana na mafundisho ya dini hiyo
badala ya kundi la watu fulani kujiona ni bora zaidi ya kundi jingine.
‘’Sisi
sote tunafuata mafundisho ya Kitabu cha Koran na Hadithi za Mtume Muhammad
(SAW) anayefuata mafundisho haya kwa dhati hawezi kukurupuka na kukejeli
wengine,’’alisisitiza na kuongeza.
‘’Wanaohoji
kwa nini tunaswali leo, tunasema kuwa sisi tunaswali mwezi wa Kimataifa ambao
dunia nzima wanaswali,wale watakaoswali kesho hakuna anayewazuia na wala
ninyi msiwakejeli ambao leo bado wamefunga na wao hawapaswi kuwakejeli ninyi
ambao leo mnakula mchana,’’alisema.
Kwa
upande wake Shekhe Rajab Nzunda alisema kuwa Waislamu wanapaswa kufuata na
kuendeleza mafundisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo wengi waliamua
kuacha maasi na kujikita katika ibada.
‘’Mwezi
wa Ramadhani umetufundisha, uchamungu, hatupaswi kurejea tena katika maovu ambayo
yalitakaswa na Mwezi huu,tusirejee tena kufanya madhambi, tuendeleze ibada na
uchamungu tuliodumu nao kwa mwezi mzima,’’alisema Shekhe Nzunda.
Matukio na Picha ni Mwenda Pole na Upole Wake Blog.
0 comments:
Post a Comment