Serikali imeombwa kuiondolea kodi inayoKitoza kiwanda cha konyagi cha Tanzania Distileries Limited (TDL), kutokana na ununuzi wa zao la zabibu kwa kuwa bado
hakijajiimarisha kiuzarishaji.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi
Mtendaji wa kiwanda hicho Bw.David Mgwassa wakati wa mkutano na waandishi wa habari
uliofanyika Dar es Salaam ambapo alielezea wasiwasi wa zao hilo kuja kudorora iwapo
kodi hiyo itaendelea kutozwa.
Alisema kutokana na uendeshaji wa
kampuni kwa miaka sita tangu ifufue mashamba ya zabibu miaka saba iliyopita kwa
kuagiza mbegu kutoka Afrika Kusini ni kipindi kifupi kuanza kukatwa kodi.
“Kipindi cha miaka sita kuanza kukatwa kodi ni mapema mno kwani bado
hatujasimama sawasawa tunaomba serikali kuangalia kwa makini jambo hilo ili
kunusuru kilimo cha zao hilo na kuwakomboa wakulima” alisema Mgwassa.
Hata hivyoalisema kuwa TDL kwa mwaka huu imenunua lita
milioni 1.720 za zabibu na kuwa lita milioni 1.1 ni kwa ajili ya kinywaji cha
Valuer na 0.7 zilienda kwenye bidhaa nyingine.
Mgwassa alibainisha kuwa mwaka jana
kampuni hiyo ilitumia sh.bilioni 1.8 kwa ajili ya kununua zao hilo ambapo mwaka
huu watatumia bilioni 2.3 na kuwa hali ya kilimo cha zao hilo ni nzuri
pamoja na soko lake tofauti ni inavyodaiwa na baadhi ya watu.
Aidha aliongeza kwa kusisitiza kwamba iwapo serikali itaendelea
kotoza kodi hiyo upo uwezekano wa vinywaji vinavyozarishwa na kiwanda hicho bei
yake kuwa juu kutokana na bei ya soko kulingana na ile ya vinywaji kutoka nje
ya nchi.
0 comments:
Post a Comment