Image
Image

NDOTO ZA KIZURI KUPAA KIMATAIFA.


                    Mussa Kizuri Mwanafunzi Tsj.



Moja ya mwanafunzi wa chuo cha uandishi wa Habari Tsj aliyekutwa na kamera yetu leo hii wakati akifanya kipindi ndani ya studio hiyo Bwana Mussa Kizuri, amesema anandoto za kufika level za kimataifa kwa namna moja ama nyingine.

Mwanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari tsj Mussa Kizuri  amesema anategemea kufanya kazi kimataifa zaidi kwani inawezekana mtu ukijituma.

Mapema leo mwanafunzi huyo aliyeko semester ya 4 chuoni hapo amesema kuwa wengi wamekuwa waoga kuthubutu kwa kuhofia kuwa hawawezi jambo ambalo yeye analiona kuwa sio jambo la kweli huku akisema.” Naamini tukijituma tunaweza kwani hakuna aliyezaliwa akiwa anajua kwamimi naamini nitafika mbali sana na kufanya kazi hadi kila mtu ashangae”alisema kizuri.
Mbali na kuwa mtangazaji mwenyekuwa na malengo ya kuvuka ng”ambo, bado ni mwanamuziki wa Hip Hop nchini Tanzania ambaye anasema yuko mbioni pia kutambulisha ngoma zake mpya katika vituo mbali mbali vya radio nchini Tanzania, ambapo alisema kuwa wakati akitaka kachia ngoma zake hizo ataweka bayana ngoma yakwanza itakwenda kwa jina gani kwani kwa sasa ni mapema mno kuitambulisha ngoma ila mashabiki wa Hip hop wakae mkao wa kula 2.

Mtangazaji huyu na mwanamziki mwenye malengo yakufika mbali alishafanya kazi na radio nyingi nyigi lakini kubwa alikaa na kufanya na Radio Kifimbo iliyopo Makao makuu ya Tanzania Dodoma.
Tambarare halisi licha yakuona mambo aliyonayo kijana huyu lakini ilibaini kitu cha utofauti kwake ambacho wengi wa watangazaji huwa wana kimbia, Suala la Production( uzalishaji) ni mtu anayeweza kutengeneza matangazo ya radi na mambo mengine mengi katika hili.

Kizuri alimalizia kwa kusema kujituma kwetu ndio msingi katika maisha na daima ukweli utaonekana kwa ulicho nacho licha yakuwa ajira zimekaliwa na watu wachache wenye mioyo ya kishetani wasio taka wengine wasonge mbele, ila anaamini kwa kumuomba muumba mambo yote yatakuwa safi kabisa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment